Home Habar za Usajili Simba ZILE TETESI ZA MUDATHIRI YAHYA KUTUA SIMBA ZIKO HIVI….MAMBO YANAENDA KIMYA KIMYA...

ZILE TETESI ZA MUDATHIRI YAHYA KUTUA SIMBA ZIKO HIVI….MAMBO YANAENDA KIMYA KIMYA AISEEE….


Kiungo wa zamani, Azam FC na Singida United, Mudathir Yahya ameingia kwenye rada za Simba ambao wapo sokoni kutafuta kiungo mpya wa ukabaji kutokana na kutolizishwa na ubora waliokuwepo sasa.

Inaelezwa mabosi wa Simba walifanya mawasiliano yenye usiri mkubwa na Mudathir ambaye kwa sasa ni mchezaji huru ila hakutoa majibu yoyote kama yupo tayari kujiunga na timu hiyo.

Mabosi hao wa Simba inaelezwa wanapambana na kutafuta kiungo mpya wa ukabaji huku, Afeez Nosiru kutokea Kwara United ya Nigeria ndio anapewa nafasi kubwa kama chaguo la kwanza kwenye usajili wa nafasi hiyo.

Mudathir kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kuachana na Azam kuna nyakati aliwahi kueleza amepanga kupumzika kucheza mpira hadi dirisha dogo la usajili ndio atafanya maamuzi timu mpya ambayo atakwenda kuichezea.

SOMA NA HII  'MAVITUZI' YA OUATTARA YAMTIA WAZIMU ZORAN...AFUNGUKA NAMNA ATAKAVYOMTUMIA KIMKAKATI KUMALIZA 'KAZI CHAFU'...