Home Habari za michezo WAKATI EDO KUMBWEMBE ‘AKIMPAKA’ BENCHIKHA….AHMED ALLY KAMJIBU HIVI….

WAKATI EDO KUMBWEMBE ‘AKIMPAKA’ BENCHIKHA….AHMED ALLY KAMJIBU HIVI….

Habari za Simba SC

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema mara baada ya Simba kuanza kufundishwa na kocha wao mpya Benchikha, mazoezi yake yanavutia.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ahmed ameweka ujumbe huo akionesha ana hamu ya kwenda kuangalia mazoezi ya Benchikha.

“Muda ufike tuu tuende mazoezini siku hizi raha kweli kuona mazoezini yetu. Raha unayoipata kuiona Simba ya Benchikha ni kama kupokea mshahara au kuvunja kikoba.”

Aidha katika hatua nyingine,Mchambuzi wa soka nchini Edo Kumwembe amesema, tabia au hulka ya viongozi wa Simba na kocha wao mpya Benchikha zinafanana sio watu wa uvumilivu.

Amesema Benchikha akiona unamzingua hakawii kukuachia timu kama ilivyo kwa uongozi wa Simba, wanasifikika kwa kutimua walimu.

“Simba na Benchikha wana tabia sawa, ndio maana unaona Bechikha kashahama vilabu vingi, Raja kafundisha mara mbili sijui hivyo wana tabia sawa,” alisema Edo.

SOMA NA HII  YANGA -TUNATAKA CHANGAMOTO YEYOTE..... ANAETUWEZA AJE...