Home Habari za michezo KWA NINI ZIMBWE Jr NI ‘MTI MKAVU’ SIMBA….UKWELI WA MAMBO UKO HIVI…JAMAA...

KWA NINI ZIMBWE Jr NI ‘MTI MKAVU’ SIMBA….UKWELI WA MAMBO UKO HIVI…JAMAA HALI KUKU KABISA…

Habari za Simba

Kila unapoona mafanikio ya mtu yoyote basi nyuma yake kuna siri ya mafanikio au njia alizotumia kufikia mafanikio yake.

Leo nataka nikupe mambo muhimu machache ya beki wa Simba SC na timu ya taifa ya Tanzania Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.

Unajua tangu Tshabalala ajiunge na Simba hajawahi kupata majeraha makubwa ya kumuweka nje muda mrefu.

Mwaka 2015 alipewa tuzo ya mchezaji aliyekuwa fiti ndani ya Simba kwa kucheza mechi za mashindano yote ya msimu bila kukosekana.

Sasa nataka kukupa kwa nini yupo fiti na hajawahi kuumia kwa kukosekana kwenye kikosi sababu ya majeraha;

1: Tshabalala anafanya sana mazoezi sana.
2: Hali kuku aina ya broiler wala mayai ya kuku wa kisasa.
3: Hanywi soda wala juice za kemikali za viwandanj, isipokuwa fresh juice tu.
4: Pia hali vyakula vya kisasa kama pizza, burger Wala vyakula vya kemikali
5: Beki huyu pia hali vyakula vya mafuta mengi anapenda kula vyakula vya chukuchuku zaidi
6: Pia Zimbwe Jr hajawahi kwenda klabu ya starehe katika maisha yake yote.

Unaweza wewe?

SOMA NA HII  JANJA JANJA YA YANGA SC KWA MASTAA WA AZAM FC YASHTUKIWA...WAPEWA 'MAKAVU LIVE'...