Home Geita Gold FC OHOO…UNAAMBIWA HUKO GEITA GOLD PAMENOGA…ACHANA NA NTIBAZONKIZA…VYUMA VINGINE VIPYA HIVI HAPA…

OHOO…UNAAMBIWA HUKO GEITA GOLD PAMENOGA…ACHANA NA NTIBAZONKIZA…VYUMA VINGINE VIPYA HIVI HAPA…


Kocha Mkuu wa Geita Gold, Fred Felix ‘Minziro’ amesema ongezeko la wachezaji wake watano wa kigeni kwenye kikosi chake umeongeza chachu ya ushindani huku akimtaja Fabrice Kayemba kuwa kuwa atamuongeza ubora George Mpole.

Minziro amefunguka hayo baada ya mastaa wao wa kigeni kupata ruksa ya kuitumikia timu hiyo baada ya ITC zao kutumwa na sasa ni uamuzi wake kuwatumia.

Mastaa hao ni Mcauther Arakaza kipa kutoka Burundi, Shown Oduro kutoka CB Acra Ghana, Fabrice Kayemba kutoka DR Congo, Saido Ntibazonkiza kutoka Burundi na Shinodu Sakai kutoka Japan.

Minziro alisema amefurahishwa na ongezeko la mastaa hao huku akikiri kuwa sasa timu yake ina mashindano mengi hivyo anahitaji kikosi kipana chenye ushindani wa namba.

“Eneo la ushambuliaji kuna George Mpole ambaye ndiye aliyeibeba timu msimu uliopita kwa kuifungia mabao mengi na kuibuka kinara ujio wa Kayemba utampa changamoto uya kuuwa bora zaidi,” alisema Minziro.

“Timu ikiwa na wachezaji zaidi ya wawili kwenye nafasi moja inakuwa na ubora kutokana na kila mchezaji kuhitaji kuonyesha yeye ni bora zaidi ya mwingine hivyo naamini nitakuwa na timu ya ushindani mara baada ya ligi kurudi.”

Akizungumzia mapumziko ya wiki mbili kupisha mechi mbili za timu ya taifa ‘Taifa Stars’ kufuzu CHAN alisema yamekuwa na faida upande wao kutokana na kuendelea kluimarisha kikosi chao ikiwa ni sambamba na kujiweka fiti zaidi baada ya kuchelewa kuanza maandalizi ya msimu.

“Tunaendelea kujifua naamini wiki hizi mbili kwa upande wetu zilikuwa na faida kwasabau hatukufanya maandalizi ya msimu vizuri kutokana na kuchelewa kuingia kambini na tutakuwa na mechi mbili za kirafiki kabla ya kumvaa Kagera Sugar na mewchi yetu ya kimataifa,” alisema.

Geita Gold baada ya kupata pointi moja kwenye mechi mbili za ligi walizocheza dhidi ya Simba walikubali kipigo cha mabao 3-0 na mechi ya pili dhidi ya Azam FC waliambulia sare ya bao 1-1 Agosti 6 watakuwa wenyeji wa Kagera Sugar.

SOMA NA HII  YANGA NA MIPANGO YA POINTI TATU ZA AL AHLY