Uncategorized

YANGA: TOWNSHIP ROLLERS TUNAWATAMBUA HAWATUTISHI, MASHABIKI WATUPE SAPOTI

admin August 6, 2019 6:07 pm


DISMAS Ten, Kaimu Katibu wa Yanga amesema kuwa kikosi kinajichimbia visiwani Zanzibar ili kujiwinda na mchezo wao wa kwanza wa awali wa kimataifa dhidi ya Township Rollers.

Yanga itamenyana na Township Rollers Jumamosi uwanja wa Taifa majira ya saa 12:00 jioni, Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ten amesema kuwa wanawatambua vema wapinzani wao hivyo kazi yao ya kwanza itakuwa ni kupata ushindi nyumbani kabla ya kwenda ugenini.

“Hii michuano ya kimataifa ina changamoto zake na kwa hatua ambayo tupo kwa sasa ni lazima tuanze kupata ushindi nyumbani hivyo tunaamini tutaanza kuchanga karata yetu vizuri.

“Mchezo wetu wa kwanza nyumbani ni muhimu kushinda na tutapambana kupata matokeo, mashabiki watupe sapoti,” amesema.

KAGERE NOMAA. ASEPA NA MPIRA WAKE LEO TAIFA MBELE YA POWER DYNAMO MABINGWA WA KOMBE LA FA AZAM FC KUWAFUATA LEO KIBABE WAETHIOPIA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply