Simba SC

UBINGWA MKOBANI, SIMBA QUEENS WAWINDA AFRIKA

Vardo June 13, 2026 2:19 pm

BEKI wa Simba Queens, Ruth Ingose, amesema kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania ni hatua muhimu kwa timu hiyo, lakini bado wana kazi kubwa ya kuhakikisha wanafanya vizuri katika michuano ya CECAFA ili kufikia malengo yao ya kimataifa.

Simba Queens tayari imetawazwa mabingwa wa ligi hiyo na kukabidhiwa kombe la ubingwa huku ikiwa bado imebakiza mchezo mmoja kabla ya kumalizika rasmi kwa msimu wa mashindano.

Ruth amesema mafanikio ya kutwaa ubingwa ni matokeo ya juhudi kubwa zilizowekwa na wachezaji, benchi la ufundi pamoja na uongozi wa klabu katika kipindi chote cha msimu.
Ameeleza kuwa moja ya malengo waliyojiwekea mwanzoni mwa msimu lilikuwa ni kutwaa ubingwa bila kupoteza mchezo wowote, jambo ambalo kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa kulifikia.

Beki huyo amesisitiza kuwa pamoja na kushinda taji hilo, bado wanahitaji kumaliza ligi kwa nguvu kwa kuhakikisha wanashinda mchezo wao wa mwisho ili kuhitimisha kampeni yao kwa rekodi nzuri zaidi.

“Tumekuwa mabingwa huku tukiwa bado na mchezo mmoja mkononi, hivyo tumefikia lengo letu la kwanza. Tunataka pia kumaliza ligi kwa ushindi ili kuonyesha ubora wetu hadi mwisho wa msimu,” amesema Ruth.

Ameongeza kuwa sasa macho yao yote yameelekezwa kwenye michuano ya CECAFA, ambapo wanalenga kufanya vizuri na kutwaa ubingwa utakaowapa tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake, jambo ambalo ni ndoto kubwa kwa klabu na mashabiki wake.

BARKER ATAKA MBADALA WA MWALIMU, SOPU APEWA KIPAUMBELE WEMA SEPETU KUTOKA KUITWA TASA HADI KUPATA MTOTO