Msemaji wa Simba SC, Ahmed Ally amesema straika Mzungu, Dejan ataendelea kuwepo klabuni hapo kwani hahusiani moja kwa moja na kocha Zoran Maki aliyefungashiwa virago mchana huu.
Akizungumza mara baada ya kufanya mkutano wa ajili ya mechi yao kesho dhidi ya KMC, Ahmed alisema, wamefikia makubaliano ya kuachana na kocha Mkuu pamoja na kocha wa viungo Sbai Karim na kocha makipa Mohamed Rachid ambao ndiyo wanahusiana.
โPackage ya Zoran ilikuwa na kocha wa viungo na kocha wa makipa. Mtu pekee ambaye kocha alimpendekeza alikuwa ni Mohamed Outara ambaye naye pia atabakia maana usaji wake hauhusiani na kocha.
โOutara ni beki mzuri na tunaendelea kumhitaji ndani ya klabu na Dejan vilevile hahusiani na kocha Zoran hata kidogo,โ alisema Ahmed.