Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo amesema begi lake ambalo lilipotea Airport, Amsterdam likiwa na viatu vyake na vifaa vingine, limepatikana, itakumbukwa usiku wa Septemba 3, 2022 Mwakinyo katika pambano dhidi ya Muingereza Liam Smith lililochezwa Liverpool, England alipoteza kwa TKO round ya 4 katika pambano la round 12 ambalo hata hivyo lilikuwa gumzo kutokana na jinsi lilivyomalizika kwa utata.
Baada ya pambano hilo Mwakinyo akasema “Hujuma ambayo imetokea juzi wakati nafika Airport Watuwote walipata mabegi Mimi langu sikulipata karibu masaa matatu nimelisubiri baadaye wakaniambia begi langu limesahauliwa Amsterdam kwahiyo nikae pale masaa matano walilete au nitoe anuani ya napokaa watalituma baada ya siku mbili”
“Niliwasiliana na Promota akaniambia njoo uendelee na mambo mengine sisi tutashughulikia masuala ya begi lako, begi halijakuja juzi, jana na leo siku ya pambano wamenipa vifaa vingine vyao, viatu ambavyo nimevaa sijawahi kuvaa kupigania kuna muda nilipiga goti nikamwambia Refa nimepata ankle akaniambia unaweza kuendelea nikasema naweza kuendelea”
“Mara ya pili nikasikia ankle inakuja tena, nikatema mouth guard chini, sheria ukitema mouth guard Refa anatakiwa amrudishe nyuma Boxer unayepigana nae akuulize kuna tatizo gani au akuhesabia nikamwambia nina ankle akamaliza pambano”
Bondia Mtanzania Mwakinyo amesema kutokana na Refa wa pambano hilo kuwa ‘unfair’ kwake, Promota Benjamin Shalom amekubali pambano hilo lirudiwe January 2023 vs Liam Smith.