Ligi Kuu

RATIBA LIGI KUU YAANZA ‘KUTIKISWA TIKISWA’…TPLB WATOA ‘KAMKEKA’ KAFUPI CHA MABADILIKO…SHOW ZIKO HIVI SASA..

admin September 15, 2022 6:39 pm


Bodi ya Ligi Kuu ‘TPLB’ imefanya mabadiko ya ratiba ya Michezo miwili ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2022/23 ambayo ilipangwa kuchezwa Septemba 16 na 17, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salam.

Timu zilizoguswa na mabadiliko hayo ya ratiba ni Ruvu Shooting ya Mkoani Pwani, Polisi Tanzania ya Mkoani Kilimanjaro, Ihefu FC kutoka Mbeya na KMC FC ya Dar es salaam.

Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi imeeleza kuwa Mchezo namba 29 wa Ligi Kuu kati ya Ruvu Shooting dhidi ya Polisi Tanzania uliokua umepangwa kuchezwa Septemba 16 katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam, umesogezwa mbele hadi Septemba 12 na utaendelea kupigwa Uwanja wa Uhuru.

Mchezo Namba 30 wa Ligi Kuu kati ya KMC FC dhidi ya Ihefu FC ulipangwa kuchezwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam Septemba 17, nao umesogezwa mbele hadi Septemba 20 na utaendelea kubaki kwenye Uwanja wa Uhuru.

TPLB imeeleza kuwa sababu za mabadiliko hayo ni kutokana na Uwanja wa Uhuru kuwa na matumizi mengine katika tarehe ambazo zilipangwa awali kwa ajili ya michezo hiyo miwili.

ISHU YA UWEZO WA FEI TOTO NA SIASA ZA ZNZ ZAMFANYA EDO KUMWEMBE KUIBUKA NA MADAI HAYA MAZITO… YANGA SC WASHTUA AFRIKA,…REKOI YAO YAWA GUMZO…MGUNDA AOMBEWA KIBALI TENA SIMBA SC…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply