Kiungo wa kimataifa wa Yanga, Khalidi Aucho raia wa Uganda aliyepata majeraha juzi dhidi ya Mtibwa Sugar, anaendelea vizuri kwa mujibu wa daktari wa timu hiyo, Shecky Mngazija ambaye amesema anaweza kutumika hata wikiendi ijayo.
โAucho amepata majeraha ya kawaida tu kwenye mchezo huo mguu ulishtuka tukaona tusiendelee kumuacha uwanjani kwasababu angeweza kupata majeraha makubwa zaidi, ndipo mwalimu akaona ambadilishe kwa ajili ya mapumziko.โ
โLicha ya kupata jeraha hilo mpaka muda huu tunaozungumza Aucho anaendelea vizuri na analeta matumaini makubwa sana na mashabiki wasiwe na wasiwasi na kiungo huyo,โ amesema Shecky Mngazija.