Home Habari za michezo BAADA YA KELELE ZA TIMU FULANI FULANI KUHONGA ILI ZISHINDE…TAKUKURU WAIBUKA NA...

BAADA YA KELELE ZA TIMU FULANI FULANI KUHONGA ILI ZISHINDE…TAKUKURU WAIBUKA NA KAULI HII ….


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) imefanya kikao kazi na wadau mbalimbali, kilichojadili matokeo uchambuzi wa mfumo wa usimamizi wa fedha za maendeleo ya mpira wa miguu kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa lengo la kuweka mikakati ya kudhibiti mianya ya rushwa inayoweza kujitokeza katika eneo hilo.

Kikao kazi hicho kimefanyika Septemba 15, 2022  jijini Dodoma, kwa kushirikisha Takukuru na wadau kutoka Wiazara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, TFF, Baraza la Michezo Tanzania (BMT) pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru CP, Salum Rashid Hamduni amesema uchambuzi uliofanyika ni kwa mujibu wa kifungu cha 7(a) na (c) cha Sheria  ya kuzuia na kupambana na Rushwa Na.11 ya mwaka 2007.

“Ustawi wa maendeleo ya mpira wa miguu hauwezi kufanikiwa bila kuhakikisha tunaimarisha usimamizi wa fedha za maendeleo yake na sekta ya michezo,amesema kwenye maelezo yake na kuongeza;

“Washiriki wa kikao kazi hiki mnatakiwa kushiriki kikamilifu mjadala na kuwa tayari kutekeleza mapendekezo ya mikakati ya kudhibiti mianya ya rushwa.”

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Uzuiaji Rushwa Takukuru, Sabina Seja amesema; “Tanzania ni miongoni mwa nchi wanachama wa utekelezaji wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa kupambana na Rushwa-UNCAC na inatakeleza maazimio ya mkataba huo ya kuzuia na kupambana  na rushwa katika sekta ya michezo.”

SOMA NA HII  SIMBA KUMTUMIA MISO MISONDO KUWAMALIZA WYDAD KWENYE LIGI YA MABINGWA AFRIKA..