Home Azam FC BAADA YA ‘KUFANYWA VIBAYA’ NA FEI TOTO JUZI…GOLIKIPA LA AZAM FC AIBUKA...

BAADA YA ‘KUFANYWA VIBAYA’ NA FEI TOTO JUZI…GOLIKIPA LA AZAM FC AIBUKA KWA HASIRA NA NENO HILI KWA YANGA…


Baada ya kuchomoa mkwaju wa penalti wa Djuma Shaban na kuokoa mashambulizi kibao ya Yanga kwenye mechi ya Ligi Kuu juzi Jumanne mechi iliyomalizika kwa sare ya 2-2, kipa wa Azam FC Ali Ahamada amefichua siri ya ubora wake kwa kusema hakuwa na presha.

Ahamada mwenye uraia wa Ufaransa na Comoro aliyewahi kuichezea Timu ya Taifa ya Vijana ya Ufaransa U-20 ameliambia Mwanaspoti aliingia katika mchezo huo akijiamini kwani amewahi kudaka mechi ngumu zaidi ya hiyo hivyo hakuwa na presha.

“Sikuwa na presha kwakuwa nina uzoefu wa kutosha na mechi za namna hii. Kwa hapa Tanzania ni mechi iliyokuwa na presha lakini kwangu niliichukua kawaida kwani nimewahi kudaka katika mechi ngumu zaidi,” alisema Ahamada na kuongeza:

“Nawapongeza wachezaji wetu kwa kujitoa na kuhakikisha hatupotezi mechi ile, pia nalipongeza benchi la ufundi nadhani mchezo huu umetupa mwelekeo sahihi wa mechi zijaozo.”

Kipa huyo wa Timu ya Taifa ya Comoro kwa sasa pia alisema malengo yake ndani ya Azam huku akiwatoa shaka mashabiki wa chama hilo juu ya ubora wao kwa msimu huu.

“Kila mchezaji anajitoa ili timu ifikie malengo na sio mimi pekee, msimu huu tunataka uwe wa furaha kwa mashabiki wa Azam na tupo tayari kupambana kuhakikisha hilo linatimia,” alisema Ahamada ambaye msimu huu ni wa kwanza kwake kucheza Ligi ya Afrika na kabla ya hapo alikuwa akicheza zake Ulaya.

Azam itacheza tena Septemba 13, 2022 jijini Mbeya dhidi ya Mbeya City katika raundi ya nne ya Ligi Kuu Bara. Wengine wapya waliong’ara Azam ni Waivory Coast, Tape Edinho na Kipre Junior, Mnigeria Isah Ndala, Mghana James Akaminko, Msenegal Malickou Ndoye na wazawa Abdul Seleman ‘Sopu’, Nathanael Chilambo na Cleophace Mkandala.

SOMA NA HII  BAADA YA KUFUNGA GOLI JUZI...MORRISO 'AANZA KUKERA' YANGA...ATUPA JIWE LA GIZANI KWA AZAM FC...