Home Habari za michezo FT: SIMBA 2-2 KMC FC….PAMOJA NA MAKI KUONDOKA ..MAMBO BADO MAGUMU MSIMBAZI…STRAIKA...

FT: SIMBA 2-2 KMC FC….PAMOJA NA MAKI KUONDOKA ..MAMBO BADO MAGUMU MSIMBAZI…STRAIKA MZUNGU ACHINJIWA BAHARINI..

[the_ad id="25893"]


Kaimu Kocha wa Simba, Seleman Matola ameanza na sare ya magoli  mchezo wake wa kwanza akiiongoza Simba tangu kuondoka kwa Kocha Zoran Maki alietimkia nchini Misri.

Simba walikua na kibarua kizito mbele ya KMC mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara mtanange uliopigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Simba waliokuwa nyumbani ndio wa kwanza kupata bao dakika ya pili kipindi cha kwanza kupitia kw Moses Phiri goli ambalo lilidumu mpaka kipindi cha kwanza kinaisha.

Kipindi cha pili KMC walimuingiza Matheo Anthony ambae dakika ya 47 akawarudisha mchezoni kwa bao ambalo walinzi wa Simba walifanya makosa.

Dakika ya 57 KMC wakapachika bao la pili na kufanya benchi la Simba kupagawa, na goli lililowafanya Simba kufanya mabadiliko na kuongeza idasi kubwa ya washambuliaji ambapo waliingia John Bocco, Kibu Denis na baadae Habib Kyombo.

Dakika ya 89 Kyombo akaandika bao la pili na la kusawazisha kwa Simba na mpaka dakika 90 zinakamilika mchezo ukamalizika kwa sare ya magoli 2-2.

Sare hii ni ya kwanza kwa KMC tangu wapande Ligi Kuu kwani katika michezo 8 iliyopita dhidi ya Simba walipokea vipigo katika mechi zote 8.

Katika Mchezo huo, Straika Mzungu, Dejan hakupata hata nafasi ya kupasha viungo, hali ambayo ni kama hakuizoea toka ajiunge na Simba kwenye dirisha kubwa la usajili.

SOMA NA HII  BAADA YA KUISHINDWA SIMBA JUZI....YANGA WAPAA KWA HASIRA ZOTE KWENDA KIGOMA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here