Home Burudani KIMEELEWEKA….PROMOTA AKUBALI OMBI LA MWAKINYO….PAMBANO KURUDIWA MWAKANIIII….

KIMEELEWEKA….PROMOTA AKUBALI OMBI LA MWAKINYO….PAMBANO KURUDIWA MWAKANIIII….


Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo amesema kutokana na refa wa pambano la jana kuwa ‘unfair’ kwake, Promota Benjamin Shalom, sasa wamefikia makubaliano ya kurudia pambano hilo na mpinzani wake, Liam Smith, Januari 23, 2023.

Usiku wa Septemba 3 2022 Mwakinyo katika pambano dhidi ya Muingereza Liam Smith lililochezwa jijini Liverpool England alipoteza kwa TKO round ya 4 katika pambano la round 12 ambalo hata hivyo lilikuwa gumzo kutokana na jinsi lilivyomalizika kwa utata.

“Kutokana na mchezo wa jana na kitendo cha Refa kuwa unfair kwangu kimemlazimu Promoter Benj Shalom kutupa nafasi ya re-match na Liam Januari 23,” ameandika Mwakinyo.

SOMA NA HII  A-Z JINSI YANGA SC WALIVYOWEKA REKODI YA HESHIMA JANA...DONDOO MUHIMU HIZI HAPA..