Home Uncategorized KAZE ASAINI DILI LA MIAKA MIWILI YANGA

KAZE ASAINI DILI LA MIAKA MIWILI YANGA


 UONGOZI wa Klabu  ya Yanga leo Oktoba 16 umemtambulisha rasmi Kocha Mkuu Cedric Kaze, ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili kuwa ndani ya klabu hiyo.


Kaze alitua Bongo usiku wa kuamkia leo akitokea nchini Canada na kupokelewa na viongozi wa Yanga pamoja na mashabiki.

Amekuja kuchukua mikoba ya Zlatko Krmpotic ambaye alifutwa kazi Oktoba 3 kutokana na kile kilichoelezwa kuwa hakuwa na mwendo mzuri ndani ya kikosi hicho.

Raia huyo wa Burundi amesema kuwa anafurahi kuwa ndani ya kikosi cha Yanga kwa kuwa anakitambua na anahitaji ushirikiano.

Mkataba huo utamfanya awatumikie Wananchi hadi 2020/22.
SOMA NA HII  VIDEO: WAZIRI MWAKYEMBE KUHUSU LIGI ITAKAVYOCHEZWA