Home Habari za michezo SHABIKI WA SIMBA ALAMBA MAMILIONI JACKPOT YA M-BET….ALIKUWA HAJUI JINSI YA KUBET…

SHABIKI WA SIMBA ALAMBA MAMILIONI JACKPOT YA M-BET….ALIKUWA HAJUI JINSI YA KUBET…


SHABIKI wa Klabu ya Simba anayeishi mkoani Arusha, Joseph Marwa, ameshinda Sh. 60,321,350 baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 12 za ligi mbalimbali duniani kupitia mchezo wa Perfect 12 wa Kampuni ya M-Bet.

Marwa ambaye ni mjasiriamali, alisema awali hakuwa na imani na michezo ya kubashiri kabisa mpaka alipofuatwa kukopwa fedha ya nauli na mmoja wa washindi Kampuni ya M-bet.

Alisema kuwa mshindi huyo alimfuata kumkopa nauli ya kwenda Dar es Salaam na kuahidi angemrudishiwa baada ya kupokea fedha alizoshinda.

Alifafanua kuwa kwa vile alikua pamoja na kumfahamu mshindi huyo, bado alikuwa anasita kumkopesha kwani kipindi hicho hakuwa na imani na michezo ya kubashiri.

“Nilimpa Sh. 150,000 mshindi na rafiki yake ambao walikuja Dar es Salaam kufuata fedha hizo. Sikuwafuatilia kabisa kwa sababu walikuwa vijana ninaowafahamu, lakini baada ya kurejea, kijana alinirejeshea fedha yangu na kwa kuongeza Sh. 50,000 zaidi.

“Sikuamini kabisa na kuanza kumhoji maswali kadhaa na baadaye kumwomba anifundishe kuweka mkeka. Alifanya hivyo na siku ya kwanza tu tokea kuanza kubashiri, nilishinda 800,000 na zaidi ambazo nilitumiwa kwenye simu,” Marwa alisema.

“Tokea hapo nikaanza kubashiri na M-Bet na kushinda fedha mbalimbali kabla ya kuibuka mshindi katika Jackpot.”

Marwa pia aliwapa rai vijana wenye umri kuanzia miaka 18 kuacha kutumia Sh. 1,000 kununua sigara na kuvuta wakati wanaweza kuzitumia fedha hiyo kubashiri na M-Bet na kujishindia mamilioni ya fedha kama yeye.

Mkurugenzi wa Masoko wa M-Bet, Allen Mushi, alisema Marwa anakuwa mmoja wa wanachama wa nyumba yao ya mabingwa kwani ni mshindi wa tisa wa Jackpo tokea kuanza mwaka huu.

“Tunaposema M-Bet ni nyumba ya mabingwa, tunakuwa na maana maalum, mpaka sasa tumewazadia mamilioni washindi nane na wameweza kubadili maisha yao,” alisema Mushi.

SOMA NA HII  KIUNGO WA YANGA MAMBO MAGUMU