kimataifa

BAADA YA KUBEBA TUZO YA Ballon D’Or JUZI…BENZEMA ATAJA TIMU ATAKAYOSTAAFIA SOKA…

admin October 19, 2022 4:52 pm

Staa wa klabu ya Real Madrid na timu ya Taifa ya Ufaransa Karim Benzema, amesema anapanga kustaafia Madrid kwa kuwa haoni nafasi ya kwenda mahala pengine.

Staa huyo mshindi wa tuzo ya Ballon D’or amezungumza hayo katika hafla ya ugawaji wa tuzo hizo jana usiku wakati akiibuka mshindi wa tuzo hiyo pale alipoulizwa na mwandishi wa habari kuhusu hatma yake ndani ya klabu hiyo.

“Nimepanga kustaafu hapa Real Madrid. Hakuna sehemu nyingine ninayoweza kustaafia ndivyo nionavyo mimi” Alisema Karim Benzema.

Staa huyo ambaye anashikilia kiatu cha mfungaji bora wa ligi kuu ya Hispania pamoja na ligi ya mabingwa ulaya tayari amefikisha miaka 14 ndani ya klabu hiyo amepanga kumalizia soka lake kwenye klabu hiyo ambayo amefanikiwa kushinda mataji mbalimbali ndani ya klabu hiyo.

Karim Benzema anaona klabu hiyo hiyo kama sehemu pekee ya kumalizia soka lake kwasababu ndio klabu kubwa kabisa duniani hivo haoni kama kuna sehemu nyingine atakwenda baada ya Real Madrid ikawa na ukubwa zaidi.

MAYELE : SUDAN PALIKUWA PAGUMU SANA…LAZIMA TUFANYE JAMBO… SIMBA QUEENS MGUU SAWA KUANZA KUITIKISA AFRIKA…CAF YAWABEBA KWENYE RATIBA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply