Home Habari za michezo BAADA YA YANGA KUTOLEWA LIGI YA MABIGWA…SHAFFIH DAUDA KAIBUKA NA HILI JIPYA...

BAADA YA YANGA KUTOLEWA LIGI YA MABIGWA…SHAFFIH DAUDA KAIBUKA NA HILI JIPYA …

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Shaffih Dauda amewapongeza Klabu ya Yanga kwa hatua waliopiga katika michuano ya Kimataifa huku akisema kuwa ni hatua nzuri kwani mafanikio hayaji siku moja.

“Naona Yanga wanakwenda vizuri, wana utulivu, wana timu nzuri, suala la matokeo ni jambo la mchakato sio jambo la kulala na kuamka hususan huku kwenye mashindano ya CAF.

“Wametolewa na Al Hilal [mabingwa wa Sudan] ni miongoni mwa klabu kubwa kwenye mashindano ya CAF. Kwa hiyo Yanga wanapaswa kukubali na kujua wapo wapi na wanaelekea wapi.

“Kwa mfano ningekuwa sehemu ya uongozi wa Yanga, kufa au kupona kwetu ingekuwa kwenye CAF Confederation Cup, tumetolewa CAF Champions League nguvu zetu tuelekeze CAF Confederation kwa ajili ya kuendelea kupata uzoefu.

“Lakini hata CAF Confederation Cup pia sio mashindano mepesi kwa sababu kuna timu kama Berkane, Pyramids, huku ndio nyumbani kwao,” amesema Shaffih Dauda.

Yanga walishinda mechi mbili za awali dhidi ya Zalan FC kabla ya kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Al Hial ya SUdan.

Kwa sasa Yanga imepanga kucheza michuano ya Kombe la Shirikisho na Club Africain ya Tunisia ambapo mchezo wa kwanza utapigwa Novemba 2 katika Dimba la Mkapa na marudiano Novemba 9, nchini Sudan.

SOMA NA HII  WAKATI CHUPA YA MVINYO WA SIMBA KUHUSU MABADILIKO IKIWA INACHAKAA...CHUPA YA YANGA NDIO KWANZA MPYAAA...