Habari za michezo

DAKIKA CHACHE KABLA YA KUKIPIGA NA YANGA LEO…MGUNDA AITA MASHAHIDI TAIFA…

admin October 23, 2022 1:43 pm

Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda amewaita mashabiki wa soka kwa Mkapa leo jumapili kwa ajili ya kushuhudia mchezo wa ligi kuu dhidi ya Yanga.

Mgunda ambaye amekinoa kikosi hicho kwa mafanikio makubwa atasimamia Dabi hiyo ya kariakoo akiwa kocha Mkuu kwa mara ya kwanza baada ya kukabidhiwa kikosi hivi karibuni.

Mgunda amesema kuwa mashabiki ni wachezaji wa 12 uwanjani hivyo wanapaswa kujitokeza kwa ajili ya kuongeza hamasa.

“Kama tunavyojua dabi ni mchezo mgumu sana hivyo tayari nimewaandaa wachezaji wangu kwenda kupambana ili tuweze kupata ushindi.

“Kila mmoja anatambua umuhimu wa mchezo huu, hivyo nawaomba mashabiki wa soka waweze kujitokeza kwa wingi ili kuongeza hamasa kwa wachezaji kwani wao ni wachezaji wa 12 uwanjani.”

KUWANIA KUFUZU AFCON MWAKAN..TANZANIA KAMA YANGA TU…MAMBO MAGUMU… MABEKI YANGA WAMTANGAZIA KIAMA MOSES PHIRI…WAAPA ‘KULALA NAYE MBELE’…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply