Tanzania imelazimishwa sare ya goli 1-1 na Nigeria jana jioni katika Uwanja wa Benjamin Mkapa katika mechi ya kwanza Raundi ya Pili ya mchujo wa kuwania tiketi ya AFCON U23 mwakani.
Wageni walitangulia kwa bao la penalti la nyota wa CD Diocesano ya Hispania, Success Makanjuola dakika ya 28, kabla ya mshambuliaji wa Moroka Swallows ya Afrika Kusini, Ally Msengi kuisawazishia Manyara Stars dakika ya 76 kwa penalti pia.
Timu hizo zitarudina Oktoba 27 nchini Nigeria na mshindi wa jumla atamenyana na Uganda katika mechi ya mwisho y mchujo ya kuwania tiketi ya AFCON U23 mwakani.
SOMA NA HII WAKATI AZIZI KI AKISINYA MKATABA MPYA YANGA....NABI, WYDAD WATIA DAU KUMCHOMOA PACOME...