Home CAF KISA USHINDI WA SIMBA JANA…RAIS SAMIA ATUMA KONGOLE MSIMBAZI…YANGA WACHUNIWA…..

KISA USHINDI WA SIMBA JANA…RAIS SAMIA ATUMA KONGOLE MSIMBAZI…YANGA WACHUNIWA…..

Rais Samia Suluhu Hassan, amewapongeza Simba SC kwa kufanikiwa kutinga hatua ya Makundi ya Klabu Bingwa Afrika.

Simba ilitinga hatua hiyo jana Oktoba 16, 2022 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar baada ya kuwafunga goli moja kwa bila vijana wa Agosto kutoka Angola.

Kupitia ukuara wake wa Instagram ambao upo varrified, Rais Samia aliposti picha ya kikosi cha Simba na kusindikiza na ujumbe wake wa pongezi.

“Kongole @SimbaSCTanzania kwa ushindi wa 1-0 (ushindi wa jumla 4-1) mlioupata dhidi ya timu ya Primeiro De Agosto ya Angola na hivyo kufanikiwa kuingia hatua ya makundi ya klabu bingwa Barani Afrika. Nawatakia kila kheri katika michuano inayofuata.”

Katika mchezo wa awali uliopigwa nchini Angola, Simba aliafinikiwa kuwapiga Agosto goli 3-1.

SOMA NA HII  ROBERTINHO ATAKA USHINDANI SIMBA, AFUNGUKA HAYA AKIWA KAMBINI