Home news WAKATI YANGA NA GSM WAKITAKA KUMPA MIL 400 …HIVI NDIVYO MO DEWJI...

WAKATI YANGA NA GSM WAKITAKA KUMPA MIL 400 …HIVI NDIVYO MO DEWJI ALIVYOFANYA KUFURU ISHU YA CHAMA….


AMINI usiamini, sasa ni wazi kuwa zile kelele juu ya usajili wa kiungo mshambuliaji wa RS Berkane, Clatous Chama, zimeisha namna hii, baada ya kuvuja kwa siri ya kwamba tayari Simba imemalizana na mchezaji huyo na tayari wamemrejesha nyumbani kwao Lusaka, Zambia.

Takriban miezi mitatu sasa, gumzo la jiji ni juu ya usajili wa Chama, ambaye alikuwa mara akihusishwa na Yanga ambao walidhaniwa kumtangazia kitita cha dola laki mbili (200,000) zaidi ya shilingi milioni mianne, ili avunje mkatabawake lakini sasa upepo wa mchezo umebadilika ghafla baada ya Chama kuvunja mkataba wake chini ya uangalizi wa mabosi wa Simba.

Chanzo makini kutoka ndani ya Simba, kimelinyetishia Championi Jumamosi kwamba, kelele zote zinazosikika juu ya Chama ni danganya toto tu, kwani tayari Chama ameshavuta kitita cha Mohamed Dewji ‘Mo’, ambazo zimemfanya kuvunja mkataba wake na RS Berkane na muda wowote atatua nchini.

“Achana na kelele za mitandaoni, zaidi naomba uniamini mimi kuwa Yanga hawana uwezo tena wa kumnasa Chama, maana ishu ilimalizika tangu Desemba 27, mwaka huu, nchini ya usimamizi wa C.E.O wetu, Barbara Gonzalez, akiwa sambamba na aliyekuwa C.E.O wetu wa zamani Crescentius Magori walimaza mchezo mzima.

“Ishu ilikuwa hivi baada ya uongozi wetu kuona habari zikizagaa juu ya Chama kukosa furaha ndani ya RS Berkane zinazidi kuwa kubwa, ulilazimika kumtafuta na kukaa naye chini ambapo Chama alitaja ukweli kutakiwa na Yanga jambo ambalo walilazimika kuandika barua ya kumuomba kwa waajiri wake hao.

“Hapa ninapokwambia hivi sasa tayari Chama yupo kwao Zambia akimalizana na familia yake na nina imani kabisa kuwa ndani ya siku mbili zijazo atawasili nchini tayari kwa kuanza majukumu na wenzake baada ya kuachana nao kwa takriban miezi sita iliyopita,” kilisema chanzo hicho.

Championi Jumamosi lilimtafuta CEO wa Simba, Barbara Gonzalez, lakini simu yake ya mkononi ilikuwa haipokelewi hadi tunakwenda mitamboni.

SOMA NA HII  ROBERTINHO AFUNGUKA MBINU ALIZOWAPA WACHEZAJI WA SIMBA