Home Habari za michezo BAADA YA KUONA KAZI YA KILA MMOJA…KIGOGO SIMBA ASHINDWA KUJIZUIA UBORA WA...

BAADA YA KUONA KAZI YA KILA MMOJA…KIGOGO SIMBA ASHINDWA KUJIZUIA UBORA WA MAYELE DHIDI YA PHIRI…


Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amemtabiria makubwa mshambuliaji wao Mzambia, Moses Phiri msimu huu wa Ligi Kuu Bara kutwaa Tuzo ya Ufungaji Bora.

Nyota huyo kabla ya mchezo wa jana wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons, alikuwa amefunga mabao matatu, akiwa sawa na mshambuliaji wa Yanga, Mkongomani, Fiston Mayele.

Mayele ambaye msimu uliopita alizidiwa bao moja na George Mpole wa Geita Gold aliyekuwa Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara, msimu huu amepania kupambana kuibeba tuzo hiyo.

Ally alisema anaamini kiwango bora alichonacho Phiri, hivyo anampa nafasi kubwa ya kutwaa Tuzo ya Ufungaji Bora katika Ligi Kuu Bara msimu huu.

Aliongeza kuwa, pia amemtabiria nyota huyo kuendelea kufunga mabao mengi katika Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya mchezo wa kwanza wikiendi iliyopita kufunga bao moja kwenye ushindi wa 2-0 ugenini dhidi ya Nyasa Big Bullets.

“Wanasimba wanatakiwa kuwa watulivu, kwani hivi sasa benchi la ufundi linatengeneza kikosi imara kitakachofanya vema katika ligi na michuano ya kimataifa.

“Ninaamini kama timu ikishasukwa vizuri, kwa maana ya kutengeneza muunganiko mzuri kati ya viungo na washambuliaji, basi mshambuliaji wetu Phiri namtabiria kuwa mfungaji bora msimu huu.

“Niwapongeze wachezaji wetu kwa kuanza vizuri ligi na kimataifa, hivyo bado wana kibarua kigumu cha kuendelea katika kiwango hicho,” alisema Ally.

SOMA NA HII  SAMATAA KUVUNA MSHAHARA WA MABILIONI HAYA KWENYE KLABU YAKE MPYA YA UGIRIKI...