Home news KUELEKEA MICHUANO YA CAF…KIGOGO SIMBA AFICHUA MIPANGO YA KIMAFYA..WAZITAKA MECHI MBILI..

KUELEKEA MICHUANO YA CAF…KIGOGO SIMBA AFICHUA MIPANGO YA KIMAFYA..WAZITAKA MECHI MBILI..


MJUMBE wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mulamu Ng’hambi, amesema wamepanga kuja na mikakati mipya itakayowawezesha kufuzu hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kauli hiyo ameitoa bosi huyo, mara baada ya droo ya makundi ya shirikisho kuchezeshwa juzi na Simba kupangwa na RS Berkane ya Morocco, USGN ya Niger na ASEC Mimosas ya Ivory Coast.

Akizungumza na gazeti la Championi , Nghambi alisema kuwa kikubwa watakachokifanya ni kushinda michezo miwili mfululizo ya kwanza katika michuano hiyo.

Simba itaanza na ASEC Mimosas Februari 13 jijini Dar, kisha Februari 20 itakwenda Niger kuivaa USGN.

“Siku zote mechi mbili za kwanza za makundi ndiyo zinaamua kama unakwenda robo fainali au hauendi.

Hata msimuuliopita, mechi mbili za mwanzo ndiyo zilichangia kutufanya tuongoze kundi.

“Hivyo kama tukishinda nyumbani dhidi ya Asec na kisha ugenini dhidi ya Gendarmerie (USGN) tutakuwa katika

nafasi nzuri ukizingatia mechi mbili zitakazofuata zitakuwa dhidi ya Berkane nyumbani na ugenini,” alisema Ng’hambi

SOMA NA HII  ILE ISHU YA CHAMA KURUDISHWA DAR WAKATI WENZAKE WAKIJIANDAA NA YANGA MWANZA KUMBE CHANZO NI HIKI...