Home Habari za michezo PAMOJA NA KUWA NA KIWANGO CHA ‘PANDA SHUKA’…LUSAJO APATA WA KUMTETEA LIGI...

PAMOJA NA KUWA NA KIWANGO CHA ‘PANDA SHUKA’…LUSAJO APATA WA KUMTETEA LIGI KUU…

Habari za Michezo, habari za Simba

Kupungua kwa kasi ya ufungaji kwa mshambuliaji wa Namungo, Reliants Lusajo wala hakumpi presha kocha wa kikosi hicho, Hanour Janza akisema kikubwa timu inapata matokeo mazuri na hilo ndilo jambo la msingi.

Janza alisema anachoangalia ni namna Lusajo anavyoshirikiana na wenzake katika kusaka matokeo mazuri ya timu ndio jambo ambalo ni bora zaidi.

“Kutofunga ni hali ya kawaida ambayo inaweza kumkuta mshambuliaji yeyote, lakini kwangu napenda zaidi kuona mchango wake kwa timu hata kama hatafunga, lakini juhudi zake zikazaa matunda kwa timu. Hicho ndicho ninachokitazama.

“Lusajo ni mmoja wa washambuliaji wazuri kwangu. Ni kweli hajafunga kama michezo minne hivi, lakini amekuwa na mchango mkubwa katika michezo hiyo ambayo hajafunga,” alisema Janza.

Kabla mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar mabao yote ya Namungo yalikuwa yamefungwa na Lusajo huku moja wakilipata baada ya Oscar Masai (Geita) kujifunga.

Lusajo kwa muda mrefu amekuwa kinara katika msimamo wa wafungaji kwa mabao yake matano, lakini sasa amecheza michezo minne bila kucheka na nyavu kwani mara ya mwisho alifunga Septemba 17 kwa mkwaju wa penalti katika ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union.

Msimu uliopita Lusajo alimaliza ligi akiwa na mabao 10 nyuma ya George Mpole wa Geita aliyeibuka mfungaji bora kwa mabao 17, huku Fiston Mayele (Yanga) akiwa na mabao 16.

Nyota huyo tangu msimu wa mwaka 2018/19 wakati Namungo ikiwa Ligi Daraja la Kwanza (sasa Championship) alikuwa mfungaji bora wa michuano hiyo akiwa na mabao 15, rekodi ambayo hadi sasa haijavunjwa licha ya msimu uliopita Edward Songo wa JKT kufikia idadi hiyo ya mabao.

SOMA NA HII  KISA SIMBA...DJIGUI DIARA AWEKWA KANDO YANGA....NABI AFUNGUKA A-Z MAMBO YALIVYO...AMTAJA SAKHO....