Habari za Simba
Habari za michezo

BAADA YA ‘KUPEWA MAKAVU LIVE’ NA WABONGO…OKRAH AWAJIBU HIVI KUPITIA TWITTER…

admin November 1, 2022 9:04 pm

Winga wa Simba SC mwenye kasi na ujuzi wa kukaa na mpira ambaye ni raia wa Ghana, Agustine Okrah ametumia mtandao wake wa kijamii kuwashukuru mashabiki zake kwa kumkosoa kutokana na makosa aliyokuwa akiwayafanya kwenye michezo iliyopita.

Okrah Magic, katika mchezo wa jana aliisaidia timu yake ya Simba kupata ushindi mnono wa magoli 5-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, ikiwa pia alihusika kwenye goli la kwanza lililofungwa na Mzamiru Yassin kabla ya kufunga bao 3 kwenye kipindi cha pili.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Okrah aliandika ujumbe maalum kwa mashabiki zake.

“Asante kwa ukosoaji na kunitia moyo kwa siku chache. Nimefurahi tumerudi kwenye njia ya ushindi. Ninajifunza kuishi, ili kuacha alama kwenye bustani. Tutafanikiwa.”

Mchezaji huyo alianza kukosolewa kwenye mechi ya dabi dhidi ya Yanga SC, baada ya kushindwa kutumia nafasi zilizokuwa na uwezekano wa kuwa magoli, lakini kutokana na kile kilichotafsiriwa na wengi kuwa ni Ubinafsi aliandika pia baada ya mechi hiyo kuwa “Kila kitu nachofanya huwa naifikiria timu kwanza”

HAWA HAPA MASTAA WA TIMU YA TAIFA WALIPATA SHAVU LA KUSAJILI UTURUKI… AHMED ALLY : YANGA WATATOLEWA TU…WANATAKIWA KUWA NA CHAMA ILI WASHINDE KESHO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply