Home Habari za michezo OKWA: TOKA NIMEJIUNGA NA SIMBA NAKUMBANA NA MAJERAHA SANA…NASIKIA MENGI TU….

OKWA: TOKA NIMEJIUNGA NA SIMBA NAKUMBANA NA MAJERAHA SANA…NASIKIA MENGI TU….

Simba ipo kambini ikiendelea kujifua kwa ajili ya mechi yao ijayo dhidi ya Singida Big Stars, huku mshambuliaji wa timu hiyo, Mnigeria Nelson Okwa akifunguka juu ya kutoonekana uwanjani na kushindwa kufanya mambo tangu atue klabu hapo.

Okwa aliyesajiliwa na Simba msimu huu akitokea Rivers United ya Nigeria, hajaonekana uwanjani kwa muda mrefu na kuzua hofu kwa mashabiki

Lakini, nyota huyo amefunguka kutoonekana kwake ni kutokana na majeraha aliyokuwa nayo na sio kwamba ameshuka kiwango kama wengi ambavyo wanafikiria.

Akizungumza Okwa alisema tangu amekuja Simba amekumbana na majeraha ya mara kwa mara tofauti na ilivyokuwa Rivers, akihisi huenda imetokana na kubadilisha mazingira aliyozoea kwa muda mrefu nchini kwao.

Okwa alisema mara ya mwisho kufanya mazoezi na wenzake ilikuwa siku moja kabla ya mechi dhidi ya Azam na siku hiyo alipata maumivu makali ya nyama za nyuma ya paja na kuenguliwa kikosini.

“Nakumbuka kabla ya kuumia nilikuwa sehemu ya wachezaji waliotarajiwa kuwepo kikosi cha kwanza, ila bahati mbaya nimekutana na changamoto hii,” alisema Okwa na kuongeza:

“Naona na kusikia mengi nikihusishwa nayo kuhusu kushuka kiwango hilo si la kweli ubora wangu haujashuka ila bahati mbaya niliyokutana nayo ni changamoto hiyo ya majeraha.

“Kama kiwango kingekuwa kimeshuka maana yake nisingekuwepo kwenye mpango wa mechi siku moja kabla ya kucheza mechi kubwa nchini dhidi ya Azam ambayo bahati mbaya tulipoteza.

“Nashukuru benchi la ufundi chini ya kocha Juma Mgunda na madaktari wamekuwa na karibu nami ikiwemo kunipa matibabu bora naamini si muda mrefu nitarejea uwanjani.”

Okwa alisema hajafanya mazoezi na wenzake si chini ya awamu tano kutokana na maumivu hayo makali nyuma ya paja.

Okwa alisema kama alicheza kwa kiwango bora Nigeria na CAF, hadi Simba kuvutiwa naye si rahisi ubora huo kupotea haraka hivi.

SOMA NA HII  BAADA YA KUIJUA YANGA NNJE NDANI...MOLOKO AIBUKA NA HILI...AITAJA AS VITA