Home Habari za michezo IWE ITAKAVYOKUWA….LAKINI MCHAWI WA YANGA NI HUYU HAPA…WASIPOJIANGALIA WATAPOTEA MSIMU WOTE HUU…
- Habari za michezo
- Habari za Yanga
- Habari za Yanga Leo
- Michezo
- Michezo Bongo
- Michezo Soka la Bongo
- news
- Yanga SC
Hatua iliyofuata Yanga ilikutana na kigingi cha Al Hilal ya Sudan yenye rekodi kubwa huku ikiwa chini na kocha mzoefu wa mechi za CAF, Florent Ibenge aliyekuwa ametoka kubeba Kombe la Shirikisho Afrika akiwa na RS Berkane ya Morocco.
Huu ni mzimu unaoitesa Yanga kwa sasa kuliko inavyofikiriwa. Mafanikio makubwa ya Simba katika mechi za kimataifa, yanawafanya Wanayanga kutaka kujilinganisha nayo na kujikuta ikwamia njiani, kwa vile hata watani wao nao walifika hapo kwa kutokwa jasho na damu kwa muda mrefu.
Kitu kingine kinachoitesa Yanga kwa sasa ni kukosa umoja wa dhati. Hakuna siri, ni lazima Yanga irudi chini na kujiuliza kipi kinakwamisha umoja ndani ya klabu yao, bahati mbaya ni vigumu kwa viongozi wao kusema lakini kuna vigogo baadhi waligoma kushirikiana na utawala wa Injinia Hersi Said katika kuisimamia timu hiyo.
Baada ya kuchukua mataji matatu Yanga ilifanya usajili kwenye dirisha kubwa wakilenga kuleta watu ambao wangekuja kuunganisha nguvu na wale waliowakuta kutengeneza timu kamili yenye ujazo wa kushindana kimataifa.
Wakiwa safarini Sudan, Yanga ilikumbana na mgogoro wa makocha wake wawili, kocha mkuu, Nasreddine Nabi na msaidizi wake, Cedric Kaze ambao walishindwa kuiva chungu kimoja.
Mgogoro kama huu uliwahi pia kuikumba Simba, lakini uliwahiwa kutatuliwa mapema baada ya Kocha Mbelgiji, Patrick Aussems akiwa na Mrundi, Masoud Djuma. Makocha hao walizinguana kwa kushindwa kuwa pamoja katika kazi zao na kuanza kuiathiri Simba.
Mgogoro wa makocha hao wa Yanga ulizalisha makundi ndani ya kikosi hicho, wachezaji ambao walikuwa hawapati nafasi ya kucheza walikimbilia upande wa Kaze na wengine kukaa upande wa Nabi. Mgogoro ambao ulikuwa unaendelea kuitafuna Yanga ndani kwa ndani.
Hivi karibuni kukaibuka madai mengine kuwa lipo kundi la wachezaji linadai ada za usajili baada ya kuongeza mikataba mipya wakiwemo mastaa wakubwa ambao nao baada ya kuonekana ahadi wanazopewa hazitimii walianzisha migomo baridi wakikosa hata vipindi vya mazoezi na hata kwenda kwenye mechi bila morali ya kutosha.
Yanga itolewe au isitolewe dhidi ya Club Africain lakini viongozi wanapaswa kujitathimini na mfadhili wa klabu hiyo anapaswa kukaa mezani na baraza la wadhamini kuangalia upya uti wa mgongo wa klabu hiyo kiuongozi na mambo yanavyokwenda kisha kujisahihisha kabla hawajapotea zaidi.
Mmezaliwa na kukulia katika maisha ambayo always yanawalazimisha kuwa wa mbea,mimi ni mkristo lakini katika dhambi ambazo zimetajwa kama tatizo kwa wanadamu ni kukosa upendo.Na hili tatizo limekuwa chanzo cha dhambi zote.Ndugu mwandishi pamoja na maadili ya tathnia yako kukupiga chenga hapa unajitahidi siyo kujenga ni kubomoa na kuwagawa Yanga,kumbuka kabla mechi ya KMC VS YANGA ulitoa taarifa za NABI kuondoka wakakuwahi unachozidi kufanya ni kutaka kushinikiza yale uliyoambiwa bila kujali kwa muda huu yanajenga au yana bomoa,hapa utasingizia ndiyo uandishi wa habari but ingekuwa Simba au TFF huwa mnakaa kimya na mna rely na taarifa za wasemaji wao.nakusaidia kwenye biblia ISAYA Isaya 33
1 Ole wako uharibuye ila hukuharibiwa, utendaye hila wala hukutendwa hila! Utakapokwisha kuharibu, utaharibiwa wewe; na utakapokwisha kutenda kwa hila, wao watakutenda hila wewe.