Habari za michezo

OKWA: YANGA WAKITOBOA KESHO KUTWA ..MJE NIMEKAA PALEE…

admin November 7, 2022 8:26 pm

Kikosi cha Yanga kiliochopo nchini Tunisia kwa pambano la marudiano la mtoano wa kuwania kuingia makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji wao, Club Africain, lakini kiungo mshambuliaji wa Simba kutoka Nigeria ameuchambua mchezo huo wa Jumatano.

Yanga ililazimishwa suluhu na Africain katika mechi ya kwanza iliyopigwa katikati ya wiki hii na sasa inalazimika kusaka sare yoyote ya mabao au ushindi ili irejea rekodi ya mwaka 2016 na 2018 ilipotinga makundi ya michuano hiyo kupitia hatua ya play-off baada ya kutolewa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Hata hivyo, wakati Wanayanga wakiwa wapo fifte fifte juu ya timu yao baadhi wakiamini ni kama imeshatolewa na wengine wakijipa moyo huenda ikatoboa, Nelson Okwa wa Simba amevunja ukimya na kuichambua Yanga kabla ya mechi hiyo.

Okwa alisema kuwa, kabla ya kujiunga na Simba aliyokuwa anaifuatilia kupitia mitandao ya kijamii, anaifahamu Yanga kutokana na kukutana nayo kwenye michezo miwili Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita akiwa na Rivers United na kuitoa kwa jumla ya mabao 2-0.

Mnigeria huyo alisema kwa msimu huu Yanga imeonekana kuimarika na kuleta ushindani katika ligi ya ndani ila kwa anga za kimataifa bado sana na inapaswa ijipange upya kwa misimu ujao na sio sasa.

“Kwenye mashindano ya CAF, si rahisi kufanikiwa kwa mara moja, unahitaji kupitia hatua kwa hatua na Yanga lazima ijue haiwezi kwa sasa, kwani hata Simba haikufanikiwa na kuwa kubwa kwa mara moja, walipambana kufika huko,” alisema Okwa na kuongeza;

“Kwa mashindano ya ndani wachezaji wa Simba kabla ya msimu kuanza tumekuwa tukihamasishana wenyewe kwa wenyewe hatutakubali kuona Yanga wanatawala tena.”

KISA KIWANGO CHA OKRAH…SIMBA WAKOSA MAMILIONI KUTOKA FIFA…WANGELAMBA BINGO NONO… IWE ITAKAVYOKUWA….LAKINI MCHAWI WA YANGA NI HUYU HAPA…WASIPOJIANGALIA WATAPOTEA MSIMU WOTE HUU…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply