Kocha Msaidizi Simba SC
Habari za michezo

KUELEKEA MECHI YA KESHO..SIMBA WATAMBA NA LENGO LILE LILE LA ‘KUSAFISHA JALALA’…

admin November 8, 2022 8:56 pm

Kocha Mkuu Juma Mgunda, amesema maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Big Stars utakaopigiwa kesho saa 10 jioni katika Uwanja wa Liti yamekamilika.

Mgunda amesema wachezaji wote waliosafiri wako kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo huo ambao malengo yao ni kuhakikisha tunapata alama tatu ugenini.

Mgunda ameongeza kuwa anaamini mchezo utakuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani hasa wanapokuwa nyumbani lakini tumejiandaa kikamilifu kufanya vizuri.

“Maandalizi ya mchezo yamekamilika, tayari tumefika mkoani Singida wachezaji wako kwenye hali nzuri, tunaamini itakuwa mechi ngumu na tutapata upinzani mkubwa,” amesema Mgunda.

Kwa upande wake nahodha msaidizi, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema ingawa tunakutana na timu ngumu lakini tupo tayari kuhakikisha tunapambana kushinda ili kuwapa furaha mashabiki wetu.

“Simba ni timu kubwa na tunajua tunaenda kukutana na timu imara kwa hiyo tumejipanga kuhakikisha tunapata matokeo ya ushindi,” amesema Zimbwe Jr.

PAMOJA NA YANGA PIA KUWA UARABUNI…DEWJI ATAKA SIMBA QUEENS WAPEWE BENDERA YA NCHI…. WALIOFUNGWA GOLI 7 BILA WAIPA YANGA MBINU ZA KUIFUNGA CLUB AFRICAIN KESHO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply