Mfadhili wa zamani wa Klabu ya Simba, Azim Dewji ameipongeza Simba Queens baada ya kutinga hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika upande wa Wanawake.
Timu hiyo imeingia hatua ya nusu fainali baada ya kufunga 2-0 Green buffaloes.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Dewji amesema kitendo walichofanya timu hiyo ni kikubwa na historia kwa nchi.
“Timu ya wanaume na wanawake zote zinafanya vizuri ni jambo la kujivunia kwa sababu wanaipeperusha vizuri bendera ya nchi,” amesema Dewji.
Dewji aliomba ubalozi wa Tanzania nchini Morocco uipe Simba Queens bendera ya nchi kwani ana imani kubwa itavuka hatua hiyo.
“Mechi iliyopita niliangalia hawakuwa na bendera lakini nazani wanaweza kuwapa bendera mbili au tatu halafu wakazipeperusha wakipata matokeo.”
Timu hiyo itacheza mchezo wa nusu fainali na Mamelod Sundown ambao ndio mbingwa watetezi wa kombe hilo.