Home Habari za michezo ONYANGO ASHTUA SIMBA…AJITENGA NA WENZAKE…AKATAA KUPANDA BASI LA TIMU..

ONYANGO ASHTUA SIMBA…AJITENGA NA WENZAKE…AKATAA KUPANDA BASI LA TIMU..

Habari za Simba SC

Beki wa kati Simba, Mkenya Joash Onyango ameduwaza wenzie mazoezini huku ikielezwa kuwa anachofanya ndicho kilichomrejesha kwenye ubora wake na kutetea namba yake.

Staa huyo anayewania namba na Kennedy Juma na Mohammed Ouattara, amekuwa na programu binafsi ya mazoezi ya ndani na nje ya Uwanja ambayo imelifurahisha benchi la ufundi lakini baadhi ya mastaa wamekuwa wakimshangaa na kutamani kufuata nyendo zake.

Mchezaji huyo aliyedumu Simba kwa miaka mitatu, imebainika kwamba akiwa kambini baada ya mazoezi jioni Uwanja wa Mo Simba Arena uliyopo Bunju yeye huwa anajiongeza. Hatumii gari la pamoja na wachezaji wenzake kurejea kambini Mbweni bali maranyingi huwa anakimbia kutoka hapo hadi kambini na haonekani kuchoka licha ya kwamba wengine wanakuwa wako hoi baada ya programu ya Juma Mgunda.

Kwa Onyango imekuwa ni tofauti mbali ya ratiba hiyo ya kukimbia huku akiwa amevaa mavazi maalum ya kufunika uso kuepuka usumbufu wa mashabiki njiani, pia kama mazoezi hufanyika asubuhi gym au uwanjani yeye baada ya hapo hujiongeza pia.

Simba ikifanya asubuhi, Onyango hurudi na wachezaji wenzake kambini baada ya kufika kabla hajaenda chumbani kwake kupumzika anatenga muda wa kufanya mazoezi mbalimbali ya gym iliyopo ndani ya kambi yao baada ya hapo anaenda kupumzika au kuendelea na ratiba ya timu.

Mazoezi ya gym iliyopo kwenye kambi hiyo si kwa Onyango tu bali wachezaji wote hupenda kufanya mazoezi na wengine wakimaliza wanakwenda kuogelea kwenye bwawa lililopo karibu na jengo hilo lenye gym.

Onyango kama Simba ikiwa imefanya mazoezi asubuhi, wakiwa kambini huomba ruhusa kwa viongozi wake wa benchi la ufundi akakimbie kwenda na kurudi kutoka Mbweni hadi Tegeta ambapo ni makadirio ya saa 2 na dakika 30 kwenda na kurudi kwa miguu.

Akirudi anaendelea na ratiba ya timu ikiwemo kula kisha anakwenda chumbani kwake kupumzika ingawa inafahamika kwamba akiwa nyumbani kwake si rahisi kukutana nae akikatiza mitaani au kwenye maeneo ya starehe kama ilivyo kwa baadhi ya mastaa wa hapohapo Simba pamoja na Yanga na Azam.

Uchunguzi unaonyesha kwamba tangu aje Simba, akiwa nyumbani muda mwingi hupumzika pamoja na familia yake na kama si asubuhi basi jioni huwa anafanya mazoezi magumu binafsi kukimbia barabarani kwa umbali mrefu au nyakati nyingine kwenda kwenye fukwe za bahari.

Mashabiki huwawia ngumu kumtambua Onyango akiwa anakimbia barabarani kwani maranyingi huwa ni usiku na anavaa nguo pamoja na kofia zinazomkinga uso wake usionekane.

Alipoulizwa Onyango kuhusiana na ratiba hiyo na maisha yake ndani ya Simba alisema kwa sasa anaendelea vizuri kwa ajili ya kuipigania timu kupata matokeo mazuri na kutoa mchango wake kwa asilimia zote zaidi ya kipindi cha nyuma.

“Kuhusu kurejea kwenye ubora baada ya changamoto zilizotokea mwanzoni mwa msimu na hilo la mazoezi binafsi ni vyema nikiyazungumzia baada ya kucheza mechi muhimu na Singida,” alisema Onyango kwa kifupi na Mwanaspoti linajua kwamba hata kesho ataanza.

Kocha Juma Mgunda, naye hakuwa tayari kuingia kiundani akidai kwamba hayo ni maisha binafsi ya mchezaji ambayo anapaswa kuyazungumzia mwenyewe.

Kwa upande wa kocha wa zamani wa Dodoma Jiji, Masoud Djuma alisema Onyango ni aina wachezaji wenye kutambua uwezo wao na kufahamu yupo Simba kwa ajili gani si rahisi mchezaji anawekwa nje kisha anagoma kutokana na jambo hilo.

“Lilikuwa si jambo rahisi kwa Onyango kuonyesha bado anastahili kucheza kikosi cha kwanza hata nafasi aliyopewa amekuwa akifanya vizuri kila mchezo, kiwango chake kipo juu,” alisema Djuma na kuongeza;

“Suala hilo la kufanya mazoezi yake mengi binafsi inaonyesha ni kiasi gani bado anatamani kucheza kikosi cha kwanza, bado ana wivu wa kufikia mafanikio mengine kwa kuonyesha kiwango bora.”

Simba inashika nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 17, ipo Singida kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya wenyeji wanaoshika nafasi ya nne wakikusanya pointi 17 unaochezwa kesho Jumatano kwenye Uwanja wa Liti. Mwanaspoti. Kata kiu ya michezo na bur

SOMA NA HII  BAADA YA TAARIFA ZA KUTAKIWA NA SIMBA KUWA NYINGI...KIBWANA SHOMARI ASHINDWA KUJIZUIA..ATOA KAULI..