Home Habari za michezo PAMOJA NA YANGA KUFUZU MAKUNDI JANA..MSIMU UJAO ISHU YA TIMU NNE CAF...

PAMOJA NA YANGA KUFUZU MAKUNDI JANA..MSIMU UJAO ISHU YA TIMU NNE CAF ITAKUWA HIVI…

CAF

Na: Hashim Mbaga 10/11/2022

Tanzania katika Msimu huu 2022-2023 Tumewakilishwa na Timu Nne za Yanga, Simba, Azam na Geita Gold baada ya kupata nafasi kutokana na Point zilizozalishwa huko nyuma zilizoishia msimu uliopita wa 2021-2022 ambako Tanzania ilikusanya Point 30.5 zilizofanya kuwa nafasi ya 11 kati ya 12 bora na mgawanyo wa Point hizo ukitokana na mjumuisho toka Timu za Yanga 0.5, Simba 28 na Namungo 2.

Mpaka Hatua ya sasa Group Stage msimu huu Tanzania imeweza kuingiza Timu mbili Simba na Yanga katika Mashindano yote ya CAF Interclub kwa maana Simba yupo Champions League na Yanga yupo Confederation Cup hatua hii sasa Itaamuliwa 16/11/2022 kwa kufanyika Draw ya kupanga Timu zote katika mashindano yote na kujua katika Group Stage inayoanza February 2023 Kila Timu itacheza na Timu gani.

MSIMU UJAYO WA 2023-2024 CAF INTERCLUB

Kwa mujibu wa Kanuni na Taratibu za Mashindano ya CAF ili kupata nafasi ya kushiriki Timu 4 ni lazima uwe katika Mataifa bora 12 ya kwanza ambayo yanapatikana kutokana na uwakilishi mzuri ndani ya miaka Mitano kwa Timu zako baada ya kuingia Group Stage.

Tanzania katika Msimu ujayo inapaswa kuanza na Point 21.5 zilizokusanywa na Timu za Simba 20 na Namungo 1.5 kufanya kushika nafasi ya 10 kati ya 12 mbele ya Guinea na Nigeria bila kuangalia ongezeko la Point zinazopatikana msimu huu kwa Yanga na Simba kuingia Group Stage na ingekuwa ngumu sana nafasi yetu kama tusingeingiza Timu msimu huu maana kuna Mataifa ya Chini kama Cameroon, Ivory Coast, Congo, Uganda na Mali wanaitafuta nafasi.

TANZANIA SASA HIVI NAFASI YETU.

Kutokana na Simba na Yanga kuingia Group Stage tu kunafanya Msimu ujayo kuanza kuongezeka Point toka 21.5 tulizopaswa kuwa nazo na sasa kuwa na Point 29 kwa ongezeko la Point 7.5 toka kwa Simba 5 na Yanga 2.5 na kufanya jumla kila timu kuchangia uwakilishi huu kwa jumla ya Simba 25, Yanga 2.5 na Namungo 1.5 na kuwa Point 29.

Hii tu imetufanya kupanda ngazi kuwa Taifa la 9 kati ya 12 bora na kutuweka katika nafasi ya zaidi ya 75% kwenda tena katika uwakilishi wa Timu Nne msimu ujayo.

Tukumbuke Point hizi za sasa hazina manufaa ya sasa ni kwa msimu ujayo na ili kujihakikishia Tanzania kushiriki nafasi 4 tena tunahitaji Point zaidi kuanzia 7-10 ambazo zinaweza kupatikana kwa Timu zote mbili kushika nafasi ya 3 sio ya mwisho katika kundi lake bila ya kwenda Quarter Final.

WAPINZANI WETU NI KINA NANI

Katika Utaratibu na mataifa 12 bora Tanzania tupo nafasi ya 9 kwa Point 29 ina maana wanaotufuata ni Libya 28, Guinea 24 na Nigeria 17.5 zote hizi zina Timu katika Group Stage.

Na kule chini nje ya Mataifa 12 bora kuna Nchi za Cameroon 16, Ivory Coast 8.5, Congo 7, Uganda 5 na Mali 4.5 zote hizi zina Timu Group Stage na zinatafuta nafasi kwenda juu.

Katika Mataifa haya Manne Libya (Al Akhdar) na Nigeria (Rivers United) zenye timu Confederation Cup wakati Guinea (Horoya) na Cameroon (Coton Sports) zenye Timu Champions league ikitokea Timu/Taifa mojawapo tu kutoingia Quarter Final Tanzania tutakuwa na 95% kushiriki tena Timu 4 msimu ujayo.

Mataifa mengine Manne ya Ivory Coast (Asec) , Congo ( Diables Noirs ) na Mali ( Real Bamako ) katika Confederation Cup na Uganda (Vipers) katika Champions League hawa wote mpaka Timu zao zifike hatua ya kucheza Fainali ndio wanaweza kuitikisa Tanzania tena bila ongezeko la Point yeyote toka 29 zilizo sasa tukiongeza 7.5 tu zote hizi zimefutika kwetu.

HITIMISHO

Droo ya Group Stage CAF Interclub itafanyika Cairo Egypt 16/12/2022 mchana kwa saa za Tanzania na Kinyanganyiro cha Kucheza kitaanza mwakani February hadi April 2023 kwa mechi 6 ambazo 3 home na 3 away.

Tanzania ili kuwa salama na uwakilishi mfululizo timu 4 ni lazima Timu zetu za Simba na Yanga zijiandae vizuri na kupata na kuzalisha Point za ziada kuanzia 7.5 hadi 10 tu.

Suala la Timu zipi zinafaa au kutosha Kushindana huko nchi isiwe kushiriki ni jukumu letu wenyewe maana maana Nafasi tunapata ila zinatuelemea kutokana na ubora wa timu zetu wenyewe kuwa tofauti na mahitaji.

KILA PENYE NIA NJIA HUONEKANA

Hashim Mbaga

0764 100001

SOMA NA HII  BAADA YA KIMYA KIREFU....MZEE KILOMONI AIBUKA NA HILI JIPYA KWA SIMBA....AMPA MAAGIZO MO DEWJI...