Home Habari za michezo PAMOJA NA KUWAITA ‘WALA MIHOGO’…INJINIA HERSI APOKELEWA KWA ‘VIBE’ YANGA ..

PAMOJA NA KUWAITA ‘WALA MIHOGO’…INJINIA HERSI APOKELEWA KWA ‘VIBE’ YANGA ..

Habari za Yanga

Pamoja na kocha mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi kutafuta njia ya kuwakwepa mashabiki wachache waliopata nafasi ya kuingia ndani ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jitihada zake zimegonga mwamba baada ya kuonekana na kuimbua shangwe kwa mashabiki wakiimba jina lake.

Nabi ndiye aliyekuwa wa mwisho kushuka kwenye ndege baada ya wachezaji na viongozi wote kutoka na kupanda ndani ya gari la timu tayari kwaajili ya kuelekea Hotelini kula na kujiandaa na safari ya kuwafuata Kagera Sugar.

Mashabiki wamemsindikiza kocha huku wakiwa wanataja jina lake hadi kwenye gari ndogo iliyokuja maalum kwa ajili ya kumpokea.

Yanga inaondoka na Air Tanzania saa moja usiku kwaajili ya kwenda Mwanza kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Kagera Sugar utakaochezwa Jumapili.

HERSI AIBUKA SHUJAA

Mbali na mashabiki kumuimba kocha pia walimtaja rais wa Yanga, Hersi Said kuwa ni kiongozi shujaa ambaye amehakikisha timu inapata matokeo pamoja na maneno mazito aliyotamkia.

Hersi alisema ushindi ni zawadi kwa mashabiki wao ambao walikuwa na maumivu makali kutokana na timu yao kushindwa kupata matokeo kwenye uwanja wa nyumbani.

“Haikuwa rahisi wachezaji walipambana na kufanya kile kilichokuwa kinatakiwa tunawashukuru na kupangeza juhudi zao sasa tumesahau matokeo yaliyopita mipango inaelekezwa kwenye mchezo ujao.” alisema.

SOMA NA HII  ADAM ADAM AFIKIRIA KUCHEZA NJE YA BONGO