Habari za Simba
Habari za michezo

RASMI: PETER BANDA NNJE YA UWANJA MPAKA MWAKANI…

admin November 15, 2022 2:00 pm

Afisa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema watamkosa mchezaji wao Peter Banda kwa miezi miwili kutokana na kupata majeraha katika mchezo wao wa NBCPL waliocheza dhidi ya Singida Big Star Fc mkoani Singida.

“Mchezo wetu uliopita pale Singida, mchezaji wetu Peter banda alitolewa nje baada ya kupata majeraha na uchunguzi wa awali ulionyesha kuwa angeweza kukaa nje kwa wiki nne, lakini leo (jana) uchunguzi wa kina umefafanyika na imbeainika atakaa nje kwa zaidi ya miezi miwili.

“Makadirio ni kwamba Peter Banda atarejea uwanjani mwezi Februari wakati michuano ya Kimataifa hatua ya makundi itakapoanza. Kwa hiyo Wanasimba watambue hilo,” amesema Ahmed Ally.

KARIA: NITAKA SIMBA NA YANGA ZIFIKE FAINAL CAF…SIMBA QUEENS WANGEBEBA KOMBE KABISA… MWAKINYO AZIDI KUPOROMOKA KIMATAIFA…HAYUPO TENA HATA KUMI BORA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply