Kaimu Kocha Mkuu wa Simba SC, Juma Mgunda, amesema kiungo wao mshambuliaji Okwa, anasumbuliwa na nyonga na ndio sababu haonekani kikosini.
Mgunda ameyasema hayo jana Novemba 18, 2022 alipokuwa kwenye mkutano wa kuelekea mechi yao dhidi ya Ruvu Shooting unaochezwa leo huku Wekundu hao wakiwa wageni.
“Nimekuwa nikisema na labda niseme tena, Okwa anaumwa. Alikuja akiwa ni mgonjwa, alituambia tatizo hilo alikuja nalo tangu kwao hivyo tumemruhusu arudi kwao kutibiwa,” alisema Mgunda.