Home Habari za michezo MATOLA:- KWA HALII….MHHH UBINGWA UTAKUWA MGUMU SIMBA….

MATOLA:- KWA HALII….MHHH UBINGWA UTAKUWA MGUMU SIMBA….

Habari za Simba Leo

Kocha msaidizi wa Simba Seleman Matola amesema kwasasa mbio za ubingwa ni ngumu kwao lakini watapambana kumaliza vyema michezo iliyosalia.

Akizungumza baada ya mchezo dhidi ya Yanga uliomalizika kwa vijana wake kuvurugwa 2-1 kocha huyo amesema bado shida yao ya kushindwa kutumia nafasi inawatafuna.

“Kuhusu ubingwa kwa sasa naweza kusema ni ngumu kuupata lakini tunaangalia zaidi mechi zilizosalia kuona tutapata nini,” amesema Matola.

Mchezo wa mwisho walipokutana katika dabi ya Kariakoo Novemba 05, 2023 Simba SC walifungwa 5-1. Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha alama 58 baada ya michezo 22 huku Simba wakisalia na alama 46 kwenye nafasi ya tatu.

Simba kesho itamenyana na wenyeji, KVZ katika Nusu Fainali ya Kombe la Muungano, Uwanja wa New Amaan Complex visiwani, ZanzĂ­bar wakati Azam FC itaanza na KMKM Alhamisi na Washindi wa mechi za Nusu Fainali watakutana katika Fainali Aprili 27 hapo hapo Amaan Complex.

SOMA NA HII  AHMED ALLY : UKWELI NI KWAMBA WYDAD CASABLANCA NI NGOMA NGUMU KWA SIMBA...