Home Habari za michezo ACHANA NA KILE KIPIGO KUTOKA YANGA …SINGIDA BIG STARS KUMBE WANAJAMBO LAO...

ACHANA NA KILE KIPIGO KUTOKA YANGA …SINGIDA BIG STARS KUMBE WANAJAMBO LAO AISEE..

Singida Big Stars

Klabu ya Singida Big Stars ambayo imepanda daraja msimu huu huku ikifanya vizuri katika ligi kuu ya NBC imetanabaisha mipango yake ya kuiwakilisha nchini mwakani kwenye michuano ya kimataifa.

Kupitia Mdau wa klabu hiyo ambaye pia ni Mbunge Festo Sanga ameweka wazi mipango ya klabu hiyo msimu huu ni kubeba ubingwa wa ligi kuu na ikitokea wameshindwa basi lengo kuu zaidi ni kuhakikisha wanaiwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa msimu ujao.

Klabu ya Singida Big Stars ni miongoni mwa vilabu vichache ndani ya ligi kuu ya NBC vyenye uwekezaji mkubwa licha ya uchanga wake, Lakini imefanikiwa kutengeneza kikosi kilichojumuisha wachezaji bora kutoka ndani na nje ya nchi.

Licha ya kupoteza kwa fedheha juzi dhidi ya mabingwa watetezi Yanga lakini klabu hiyo bado mipango yake ni kuhakikisha inaiwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa msimu ujao. Kwa maana rahisi inahitaji kua kwenye nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi.

Singida Big Stars mpaka sasa wanakamata nafasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi kuu wakiwa na alama zao 18 baada ya kucheza michezo 11. Kupitia msimamo huo mpaka sasa inaonesha bado klabu hiyo inakimbizana na malengo yake.

SOMA NA HII  RUVU SHOOTING: HATUTAFANYA MAKOSA TENA MSIMU UJAO