Home Habari za michezo KISA KAULI YA “TUNAOUMIA NI SISI”…MASHABIKI YANGA WAPIGWA MARUFUKU KUONGEA ONGEA OVYO…

KISA KAULI YA “TUNAOUMIA NI SISI”…MASHABIKI YANGA WAPIGWA MARUFUKU KUONGEA ONGEA OVYO…

Uongozi wa Matawi ya Klabu ya Yanga Mkoa wa Dar es Salaam umewapiga marufuku viongozi wake na wananchama wote kuzungumza na wanahabari kuhusu mambo kadha wa kadha yanayohusu klabu hiyo.

Hayo yamesemw jana Alhamisi Novemba 24, 2022 na uongozi wa Matawi ya Yanga mkoa huo, wakati wakizungumza na wanahabari katika makao makuu ya klabu hiyo jijini Dar es salaam.

“Tumeshakubaliana kukutana kila baada ya mechi tano, tulianza kwenye mechi ya Ngao ya Jamii tutakubaliana mengi, sisi kama wanachama wa Yanga tunatakiwa tutimize wajibu wetu ili kuusapoti uongozi.

“Tukumbuke tumepitia wakati mgumu sana baada ya mfadhiri wa awali (Yusuf Maji) kujitoa, sasa tumepata mfadhiri mwingine ambaye amejitoa kwa mengi, ametumia gharama kufanya kuleta wataalam na kufanikisha huu mchakato wa mabadiliko ambao leo tunaufurahia.

“Baada ya kutolewa katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika na Al Hilal wapo wanachama na mashabiki walianza kutukana viongozi, wachezaji na kocha, sio jambo zuri.

“Na hata tulipotoa sare nyumbani dhidi ya Club Africain wapo watu walifika mbali zaidi wakisema kocha afukuzwe, lakini sisi tulikuwa pamoja na viongozi kuwasihi wavumilie maneno hayo.

“Unamtukana kocha na wachezaji walewale ambao wanekupa ubingwa bila kufungwa, hakuna timu ambayo haifungwi, sisi tumshukuru Mungu mpaka sasa tuna mechi 48 bila kufungwa lakini haimanishi hatutafungwa, ipo siku tutafungwa.

“Tuache kuwaangusha mioyo wachezaji wetu, makocha na viongozi wetu, wanafanya kazi kubwa sana, tukubuke Yanga tulikotoka, matatizo tuliyopitia mpaka leo tunafurahi kushinda nyumbani kwa Club Africain Tunisia na kutinga makundi ya Kombe la Shirikisho, wengi hawakuamini walisema safari yetu imefika mwisho lakini leo wamefumba midomo.

“Sasa kuanzia leo, ni marufuku kwa mwananchama wa yanga kuzungumzia kuhusu masuala ya klabu, kama unazungumza wewe zungumzia masuala ya tawi lako na si klabu, masuala ya klabu tumwachie Ally Kamwe, CEO Andre na Rais Hersi.

“Masuala ya ufundi tumwachie kocha Nabi na benchi lake, utimamu wa wachezaji tumwachie daktari wa timu. Tusijifanye tunajua kila kitu, tukikubaini unafanya kinyume tutajua namna ya kukushughulikia,”

SOMA NA HII  KUELEKEA KARIAKOO DABI...AUCHO NA BANGALA WATAJWA SIMBA...MORRISON APEWA KAZI MAALUMU...