Singida Big Stars
Habari za michezo

KISA ‘KUILOGA’ SIMBA…TFF WAISHUSHIA RUNGU LA ADHABU SINGIDA BIG STARS…

admin November 27, 2022 12:33 pm

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa ligi ya Bodi ya ligi kuu Tanzania (TPLB) imemfungia mechi tatu (3) na faini ya Tsh 500,000 beki wa Klabu ya Singida Big Stars Shafiq Batambuze kwa kosa la kuingia uwanjani kupasha misuli moto kabla ya muda ulioruhusiwa.

Batambuze aliingia dakika 10 kabla kwenye mchezo dhidi ya Simba ulioisha kwa sare ya mabao 1-1 na alionekana akimwaga vitu kama maji uwanjani vitendo vilivyoashiria kuwa ni imani za kishirikina.

Maafisa wa TFF walimtaka arudi kwenye vyumba vya kubadilishia nguo hata hivyo Kocha Msaidizi wa Singida Big Stars Mathias Lule na Kocha wa magolikipa Steven Kiagundu walimuamuru aendelee kubaki uwanjani licha ya Batambuze kuanza kutoka uwanjani.

Makocha hao wamefungiwa mechi 3 na faini ya Tsh 1,000,000 kila mmoja kwa makosa hayo.

BAADA YA MASHABIKI KUANZA KUMNANGA…MGUNDA AIBUKA NA KUANIKA MSIMAMO WAKE NA SIMBA… KUELEKEA MECHI NA POLISI TZ LEO…SIMBA WAWEKA MATUMAINI KWA WAZAMBIA WAKE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply