Home Burudani BAADA YA KUKAA KIMYA MUDA MREFU…MWAKINYO AIBUKA NA NGEBE ZA KUMPIGA MZUNGU...

BAADA YA KUKAA KIMYA MUDA MREFU…MWAKINYO AIBUKA NA NGEBE ZA KUMPIGA MZUNGU ‘KAVU KAVU’…

Habari za Michezo leo

BONDIA maarufu, Hassan Mwakinyo amesema amejiandaa vyema kupambana na Peter Bobson wa Marekani katika kuwania mkanda wa WBC Desemba 30 kwenye Uwanja wa Mao tse Tung, Zanzibar.

Amesema anataka kulitumia pambano hilo kuandika historia ya kuwa bondia wa kwanza kupigana tangu kuruhusiwa mchezo wa masumbwi visiwani Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana, Mwakinyo ambaye atapigana pambano hilo chini uratibu wa promota Shomari Kimbau alisema anatumia pambano hilo kurejesha heshima yake na ya Tanzania katika uso wa dunia.

Naye Kimbau alisema Bobson kutoka Marekani yupo katika hadhi ambayo inalingana na ya Mwakinyo na kwamba anatarajia pambano hilo litakuwa na ushindani mkali.

Alisema ameamua kuliandaa pambano hilo visiwani Zanzibar ili kuandika historia ya kurejeshwa masumbwi tangu yalipopigwa marufuku.

SOMA NA HII  ISHU YA CHAMA KWENDA YANGA IMEBAKI STORI, SIMBA WAZIMA NGOMA KIBABE