Habari za Michezo leo
Burudani

BAADA YA KUKAA KIMYA MUDA MREFU…MWAKINYO AIBUKA NA NGEBE ZA KUMPIGA MZUNGU ‘KAVU KAVU’…

admin November 29, 2022 4:57 pm

BONDIA maarufu, Hassan Mwakinyo amesema amejiandaa vyema kupambana na Peter Bobson wa Marekani katika kuwania mkanda wa WBC Desemba 30 kwenye Uwanja wa Mao tse Tung, Zanzibar.

Amesema anataka kulitumia pambano hilo kuandika historia ya kuwa bondia wa kwanza kupigana tangu kuruhusiwa mchezo wa masumbwi visiwani Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana, Mwakinyo ambaye atapigana pambano hilo chini uratibu wa promota Shomari Kimbau alisema anatumia pambano hilo kurejesha heshima yake na ya Tanzania katika uso wa dunia.

Naye Kimbau alisema Bobson kutoka Marekani yupo katika hadhi ambayo inalingana na ya Mwakinyo na kwamba anatarajia pambano hilo litakuwa na ushindani mkali.

Alisema ameamua kuliandaa pambano hilo visiwani Zanzibar ili kuandika historia ya kurejeshwa masumbwi tangu yalipopigwa marufuku.

PABLO ARUDI TENA BONGO…AONEKANA NA BOSI WA SIMBA …AFUNGUK A-Z KILICHOMLETA… BAADA YA KUZINDUKA JUZI….MOSES PHIRI AFUNGUKA JAMBO ZITO SIMBA..AMTAJA JOHN BOCCO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply