Home Habari za michezo NABI AVURUGWA YANGA….AWAPIGA MKWARA WA KUFA MTU KINA MAYELE…

NABI AVURUGWA YANGA….AWAPIGA MKWARA WA KUFA MTU KINA MAYELE…

Habari za Yanga SC

Wakati Ligi Kuu Tanzania Bara ikiendelea kushika kasi, Kocha Mkuu wa Klabu ya Young Africans Nasreddine Nabi amewapiga marufuku Wachezaji wake, ili kufanikisha lengo la kuendelea kupambana kwenye michezo inayowahusu.

Young Africans kwa sasa inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na alama 32 sawa na Azam FC,

Nabi amewataka wachezaji wake kueleleza akili zao katika michezo inayowahusu na hataki kusikia mchezaji anafuatilia na kuchekelea matokeo ya wapinzani wowote kwenye Ligi wakiwemo Simba SC.

Kauli hii inawalenga mastaa wote wa Young Africans wakiwemo vinara wao, Fiston Mayele anayeongoza kwa ufungaji wa mabao hadi sasa Ligi Kuu akiwa amefunga manane, Faisal Salum ‘Feitoto’, Aziz Ki, Djigui Diarra na wengine akisisitiza anachotaka ni waangalie michezo yao na kila mchezaji ajipange kutumia mgawanyo wa nafasi za kucheza katika timu hiyo ili kuisaidia timu kushinda.

“Sidhani kama ni sahihi kwa wachezaji au sisi makocha kuanza kuangalia na kufurahia matokeo ya timu pinzani kwetu, hii nimewaambia sitaki kuona mchezaji anazungumzia hilo au kujiona tumeshinda,” alisema na kuongeza;

“Kuna mambo ambayo tunatakiwa kuwaachia mashabiki wetu kufurahia ushindi wetu au matokeo mabaya ya timu zingine. Kila mchezaji wa timu hii anatakiwa kujipanga kwa kuangalia anapambanaje kuingia kwenye timu ya kwanza ili acheze aisaidie timu hii.”

Kocha huyo bora wa msimu uliopita wa Ligi aliyechukua mataji matatu alisema ligi bado ndefu na lolote linaweza kutokea kwa kuwa mchezo wa soka yeyote anaweza kushinda.

“Nani alikuwa anajua Saudi Arabia inaweza kushinda mbele ya Argentina? Huu ndio mchezo wa soka wakati mwingine unashtua, Ligi haijamalizika tena bado ndefu lolote linaweza kutokea.”

“Tunachopaswa kufanya ni kuendelea kuhesabu kwa kushinda michezo yetu mmoja kwenda mwingine kisha tuangalie tumevuna alama ngapi mwishoni mwa msimu, hivyo ndivyo timu inayotaka ubingwa inatakiwa kuishi.”

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE