Home Habari za michezo A-Z JINSI SAKHO ALIVYOFUTA AIBU SIMBA SC JANA…IHEFU ‘WAENDELA KUBEBA WATU’…

A-Z JINSI SAKHO ALIVYOFUTA AIBU SIMBA SC JANA…IHEFU ‘WAENDELA KUBEBA WATU’…

Habari za Simba

DAKIKA 90 za mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Ihefu zimemalizika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa wenyeji kushinda bao 1-0, lililowekwa nyavuni na Pape Sakho dakika ya 63.

Ushindi kwa Simba unaifanya kufikisha pointi 21 ikiwa nafasi ya pili huku Ihefu FC ikiendelea kusalia mkiani na pointi tano baada ya timu zote kucheza michezo 10.

Zifuatazo ni dondoo muhimu za mchezo huu kwa timu hizi baada ya kutamatika kwa dakika 90.

Bao la kiungo mshambuliaji Pape Sakho ni la tatu kwake msimu huu baada ya awali kufunga mabao mawili na Mtibwa Sugar wakati Simba iliposhinda 5-0 Oktoba 30 katika Uwanja huu huu wa Benjamin Mkapa.

Tangu Ihefu FC imepanda rasmi Ligi Kuu Bara msimu wa 2019/20 haijawahi kuifunga Simba wala kutoka sare zaidi ya kuchezea vichapo mechi zote tatu walizokutana.

Mara ya kwanza zilianza kukutana Septemba 6, 2020 ambapo Simba ilishinda mabao 2-1, yaliyowekwa kimiani na John Bocco na Mzamiru Yassin huku lile la Ihefu likifungwa na Omary Mponda.

Mara ya pili kwa timu hizi kukutana ilikuwa pia katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Disemba 30, 2020 ambapo Simba ilishinda mabao 4-0, yaliyofungwa na Meddie Kagere aliyetupia mawili, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ na Chris Mugalu.

Huu ni mchezo wa tatu mfululizo kwa Ihefu kupoteza kwenye Ligi Kuu Bara baada ya kufungwa bao 1-0 na Azam FC na Singida Big Star ikiwa ni kipigo cha saba katika michezo 10 iliyocheza hadi sasa ikishinda mmoja tu na sare mbili.

SOMA NA HII  BENCHIKHA:- KWA HUYU CHAMA HUYU...EBU NGOJA KWANZA .....