Home Azam FC AJIBU AMLIZA ASUKILE…AMSHANGAA KUONA ANAVYOPOTEA KILA SIKU…

AJIBU AMLIZA ASUKILE…AMSHANGAA KUONA ANAVYOPOTEA KILA SIKU…

Tetesi za usajili bongo

Nahodha wa Prisons, Benjamin Asukile ameshangazwa kuona kipaji cha kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Ibrahim Ajibu kinapotea wakati angeweza kukipambania, akiamini hakuna timu ambayo ingeacha kumchukua nje ya nchi.

Asukile alichambua aina ya uchezaji wa Ajibu namna anavyoona nafasi za kufunga akiwa ndani na nje ya 18 na sio hilo tu bali na uwezo wake wa kuchezesha timu mbele na kuwatengenezea wengine nafasi.

Akizungumza hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Asukile alisema kitu kinachomuumiza ni kushuka thamani ya kipaji Ajibu na kupoteza vijana muhimu kwenye kikosi cha Taifa Stars.

“Ukitaja vipaji vikubwa katika nchi hii cha Ajibu ni kimoja wapo, angekuwa kwenye kiwango kikubwa hakuna timu nje ingeacha kuwania saini yake na angekuwa ghali, lakini sijui amekumbwa na nini hadi anakuwa wa kawaida sana;

“Ujue sisi wachezaji kuna muda unapenda kumuona mchezaji mwenzako mwenye kipaji akicheza, ndio maana nashangaa kwa nini Ajibu hasongi mbele, kama kuna watu waliokuwa karibu yake ambao wanaweza wakamjenga watakuwa wamekiokoa kipaji chake.”

Hilo halijamgusa Asukile peke yake, bali na staa wa zamani wa Simba, Zamoyoni Mogella aliyesema;

“Niliwahi kusema kuna wachezaji ambao wanachezea mamilioni kwenye miguu yao, ikiwemo huyo Ajibu, ana kipaji cha juu, lakini ndio hivyo huoni bidii yake kukipigania, angalau wangeiga Samatta aliyeonekana kupambana nje,” alisema.

SOMA NA HII  KIMENUKA SIMBA....SAKHO,WAWA, KISUBI NA DUNCAN HATIMA YAO SHAKANI...MAGORI AKOLEZA MOTO..