Home Habari za michezo BAADA YA KUONA HAJAPEWA NAFASI …BEKI MPYA SIMBA AVUNJA UKIMYA…MSIMAMO WAKE HUU...

BAADA YA KUONA HAJAPEWA NAFASI …BEKI MPYA SIMBA AVUNJA UKIMYA…MSIMAMO WAKE HUU HAPA..

Habari za Simba

LICHA ya kutopata nafasi ndani ya kikosi cha kwanza cha Kocha wa Simba Roberto Oliviera ‘Robertinho’, beki wa timu hiyo Hussein Kazi ameweka wazi hapa presha na aimani iko siku atapata namba na watu wataanza kuliimba jina lake.

Kazi amesajiliwa na Simba dirisha hili la usajili akitokea Geita Gold FC kuja kuongeza uimara wa safu ua ulinzi ambayo kwa sasa inaongozwa vizuri na Henock Inonga Bacca ambaye ni majeruhi na Che Fondoh Malone ameonyesha kiwango bora.

Kazi alisema anaamini muda wake wa kucheza kwenye kikosi cha timu hiyo itafikia na kuonyesha kiwango kuzuri na kumshawishi kocha Robertinho anamuamini na kumpa nafasi.

Alisema anaendelea kujifunza mambo mengi kutoka kwa wachezaji aliowakuta ndani ya kikosi cha wekundu hao wa Msimbazi, kazi yake ni kucheza mpira na ndio ulimfikisha hapo kwa hali hiyo hana presha kwa sababu Simba ni timu kubwa.

“Naamini siku yangu itafika na nitapata namba katika kikosi cha Simba hayo ni malengo yangu na ninazidi kuyapigania, kwa muda mfupi niliokuaa hapa nimejufunza mambo mengi,” alisema Kazi na aliongeza kuwa akipata nafasi atasaidia timu yake.

Alisema kwa sasa anaelekeza nguvu katika kusaidia timu kufikia malengo waliyojiwekea kushinda mataji yote ya ndani pamoja na kuvuka Robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Sina malengo binfasi kwa sasa ni timu kwanza tunahutaji kushunda mtaji yote ndani pamoja na kufanya vizuri katika ligi ya Mabingwa Afrika,” alisema Kazi.

SOMA NA HII  WACHEZAJI SIMBA WAPUNGUA MOROCCO