Home Habari za michezo DE BRYUNE: UBELGIJI INAWAZEE WENGI…HATUWEZI KUSHINDA KOMBE LA DUNIA…

DE BRYUNE: UBELGIJI INAWAZEE WENGI…HATUWEZI KUSHINDA KOMBE LA DUNIA…

[the_ad id="25893"]

Baada ya kupokea kichapo cha magoli 2-0 kutoka kwa Morocco, Kiungo wa Kimataifa wa Ubelgiji anayekipiga Man City, Kevin De Bryune haamini kama Timu ya Taifa ya Ubelgiji inaweza kubeba kombe la Dunia linaloendelea nchini Qatar.

De Bruyne ametoa kauli hiyo akiamini kuwa uwezo wa kikosi chao umepungua kutokana na wachezaji wengi wa kikosi hicho kuwa na umri mkubwa.

“2018 tulikuwa na nafasi ya kushinda kombe la Dunia ingawa hatukufanikiwa, Msimu huu siioni nafasi ya kushinda ubingwa kwa sababu asilimia kubwa ya wachezaji wa timu yetu ni wazee na mashindano yana kasi sana ” amesema kiungo huyo.

SOMA NA HII  WAKATI TETESI ZA KUUZA MECHI KWA YANGA ZIKIZIDI KUVUMA...GEITA GOLD WAVUNJA UKIMYA...WAIBUKA NA HILI...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here