Home Habari za michezo HUYU HAPA NOVATUS DISMAS MTZ ANAYEWAPAGAWISHA WAZUNGU ULAYA…KAZI YAKE NI BALAAH NA...

HUYU HAPA NOVATUS DISMAS MTZ ANAYEWAPAGAWISHA WAZUNGU ULAYA…KAZI YAKE NI BALAAH NA NUSU…

Tetesi za Usajili Yanga SC

Nguvu na akili ya mpira aliyonayo kiungo wa Kitanzania, Novatus Dismas Miroshi aliyezaliwa Septemba 2, 2002 ni miongoni mwa mambo ambayo yanamkosha kocha wake huko Ubelgiji, M’Baye Leye kwenye Klabu ya Zulte Waregem.

Leye ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu hiyo, alifichua hilo wiki chache zilizopita baada ya kuanza kumtumia mchezaji huyo wa zamani wa Azam na Maccabi Tel Aviv ya Israel kama beki wa kushoto kutokana na mahitaji ya timu.

Nafasi ya beki wa kushoto ni ya tatu kwa Novatus kutumika kwenye kikosi cha Leye kwenye mchezo wake wa kwanza Julai 23, 2022 dhidi ya RFC Seraing alicheza kama kiungo mshambuliaji, iliyofuata akacheka kama mkabaji.

“Ni mchezaji (Novatus) mwenye kipaji kikubwa ambacho kinatupa faida kwenye timu kwa kucheza kwenye maeneo tofauti, muda mwingine timu hupitia vipindi vigumu kwa kuandamwa na majerah, nafurahishwa na mwenendo wake,” anasema kocha huyo.

Akitumika kwenye nafasi yake hiyo mpya ya beki ya kushoto, Novatus alicheza kwa dakika 84 wakati Zulte Waregem ikikumbana na kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Standard Liege wikiendi iliyopita na kuwa mchezo wake wa 14 msimu huu kwenye ligi ya Ubelgiji ambayo ni maarufu kama Jupiler Pro.

Kipigo hicho ni cha pili mfululizo kwa chama la Novatus kabla ya wikiendi iliyopita kutandikwa mabao 2-1 dhidi ya KV Oostende.

Katika michezo 14 ya Novatus kwenye Ligi ya Ubelgiji ametoa asisti moja, ilikuwa kwenye mchezo wake wa tatu akicheza kama beki wa kushoto, Zulte Waregem iliibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya RSC Anderlecht.

Akizungumzia mwenendo wa timu hiyo, Leye anasema,”Hatupo sehemu nzuri kwenye msimamo wa ligi, tupo kwenye mapambano ambayo naamini yatatusaidia kuwa mbali na hatari ya kushuka daraja, mkazo wetu ni kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye michezo inayokuja tunapaswa kusahau kufanya kwetu vibaya kwenye michezo iliyopita.”

Zulte Waregem inaburuza mkia kwenye msimamo wa Jupiler Pro baada ya kushuka uwanjani kwenye michezo 15 imeambulia pointi 11 kwa kushinda michezo mitatu tu na kutoka sare mara miwili huku vipigo vikiwa 10.

Kabla ya michezo ya jana Jumapili kuchezwa, chama la nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Mbwana Samatta KRC Genk ndiyo inayoongoza msimamo wa Jupiler Pro ikiwa na pointi 40, Antwerp ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 33. Kwa upande wake, Novatus alisema hawezi kuchagua namba ya kucheza, isipokuwa ni kumsikiliza kocha wake atakamyomwamuru.

“Sina tatizo kucheza nafasi yoyote ambayo mwalimu ataona nafaa kutumika, nimekuwa nikijitoa kwa zaidi ya asilimia 100 kuhakikisha natimiza majukumu yangu kama mchezaji.”

Ndani ya michezo 14 aliyoichezea Zulte Waregem, Novatus ameonyeshwa kadi nne za njano na nyekundu ikiwa moja kwenye mchezo dhidi ya chama la zamani la Samatta, Royal Antwerp.

Miongoni mwa wadau wetu wa Nje ya Bongo, Joseph John ‘JJ’ambaye anaishi Ubelgiji ameongelea mwenendo wa mchezaji huyo wa Kitanzania ambaye alipata nafasi ya kumwona kwenye michezo miwili msimu huu ambayo ni dhidi ya KV Kortrijk na RSC Charleroi.

JJ anasema Novatus ni kati ya wachezaji ambao Watanzania watajivunia kutokana na kiwango ambacho anakionyesha huko Ubelgiji angali akiwa na umri mdogo.

“Namwona akifanya zaidi mbeleni, nilipata nafasi ya kumwona mara mbili tofauti, nilijiwekea hiyo ahadi baada ya kumshuhudia Samatta na Kelvin wakicheza kwa nyakati tofauti, Kev ilikuwa kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya upande wa vijana akiwa na Genk nakumbuka ilikuwa dhidi ya Chelsea,”

“Samatta ilikuwa akiwa na Royal Antwerp kwa mkopo ikawa amebakia Novatus ambaye ni mgeni huku, ni mchezaji mzuri sana, napenda sana namna yake ya uchezaji amekuwa akitumia nguvu na akili, kama hivi sasa anamika 20 najaribu kuvuta picha baada ya misimu miwili mitatu mbele itakuwaje,” anasema.

Zulte Waregem au kwa jina lao la utani Essevee ni klabu ya soka ya Wabelgiji ambayo mwisho wao wa juu zaidi katika kiwango cha juu ulikuwa nafasi ya pili 2012–13. Imeshinda vikombe viwili vya Ubelgiji. Ilifuzu Kombe la UEFA la 2006-07, na kupoteza katika hatua ya 32 kwa Newcastle United.

Pia, katika misimu ya 2013–2014 na 2017–2018 ilifanikiwa kucheza hatua ya makundi ya Europa.

Mara zote mbili klabu ilimaliza nafasi ya tatu kwenye kundi lake.

SOMA NA HII  BAADA YA KUCHAPWA TENA JANA...MANDONGA AIBUKA NA KALI HII MPYA...ADAI ALIPIGWA NGUMI MBILI AKAYUMBA KIDOGO...