Home news KARIA: NITAKA SIMBA NA YANGA ZIFIKE FAINAL CAF…SIMBA QUEENS WANGEBEBA KOMBE KABISA…

KARIA: NITAKA SIMBA NA YANGA ZIFIKE FAINAL CAF…SIMBA QUEENS WANGEBEBA KOMBE KABISA…

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema klabu za Simba na Yanga zilizofuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho barani Afrika zitafanya vizuri kwenye michuano hiyo na kuitetea nafasi ya Tanzania ya kuwakilishwa na timu nne.

Amezipongeza timu hizo kwa kufanya vizuri na kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo huku akizitaka kujiandaa vyema na kufika hatua kubwa ikiwamo nusu fainali na fainali.

“Tanzania sasa hivi tuko vizuri kwenye mpira wa miguu tumeheshimisha Kanda yetu ya Cecafa na kwenye uwakilishi wa klabu timu zetu zimekuwa zikifanya vizuri, katika Afrika ni nchi 12 zinazowakilishwa na timu nne na tumefanya hivyo kwa miaka mitatu, ni dhamira yangu kuhakikisha nafasi hiyo hatuiachii,”

“Ni matumaini yangu Yanga na Simba hawatatuangusha watafanya vizuri makudi na kutupa hizo pointi 10 zinazohitajika,” amesema Karia.

Karia ameipongeza timu ya Simba Queens kwa kufika nusu fainali ya Ligi ya mabingwa Afrika kwa wanawake huku akitamba kuwa alitamani timu hiyo ifike fainali na kubeba ubingwa ili mwakani Tanzania iwakilishwe na timu mbili ambapo amewaomba wadau kuwekeza kwenye soka la wanawake kwani linapiga hatua kwa haraka.

Rais huyo akiwahutubia wajumbe na wageni waliohudhuria mkutano huo amesema huu ni mwaka wa mafanikio kwa Tanzania ambapo imepata mafanikio mbalimbali ikiwamo timu ya taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 17 (Serengeti Girls) kufuzu kwa mara ya kwanza kombe la Dunia na kufika robo fainali.

Amesema Mpango mkakati wa Shirikisho hilo wa mwaka 2018-2024 moja ya malengo ilikuwa kushiriki kombe la dunia katika ngazi mbalimbali ambapo wameanza mchakato wa kuifanyia maboresho ili kupiga hatua zaidi pale ambapo malengo hayakufikiwa.

Pia amewamwagia sifa mashabiki wa soka nchini akieleza kuwa wameliheshimisha taifa huko nje na kutengeneza taswira kubwa kuhusu soka la Tanzania kwa namna wanavyojitokeza uwanjani na kuujaza uwanja.

“Kama mnavyojua ligi zetu zinazochezwa na hata mashindano ya kimataifa bila mashabiki hakuna kitu, hawa wanatuheshimisha kimataifa kwa namna wanavyojitokeza uwanjani kuziunga mkono timu zao,” amesema.

SOMA NA HII  YANGA WAONA ISIWE TABU WAMALIZANA KIMYAKIMYA NA BIGIRIMANA