Home Habari za michezo KISA KUIFUNGA ARGENTINA…MFALME SAUDI ARABIA ATANGAZA SIKU YA MAPUMZIKO NCHI NZIMA…

KISA KUIFUNGA ARGENTINA…MFALME SAUDI ARABIA ATANGAZA SIKU YA MAPUMZIKO NCHI NZIMA…

Mfalme wa Saudi Arabia, Salman bin Abdulaziz Al Saud ametangaza kuwa leo Jumatano Novemba 23, 2022 itakuwa siku ya mapumziko ya kitaifa kwa watumishi wa Serikali na Sekta binafsi pamoja na wanafunzi wote nchini humo ili kusherehekea ushindi wa bao 2-1 wa Timu ya Taifa hilo dhidi ya Argentina katika mchezo wa Kundi C wa michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Qatar.

Katika mechi hiyo iliyopigwa jana Argentina ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia mkwaju wa penati uliowekwa kimiani na nahodha wa timu hiyi Lionel Messi hadi mapumziko Argentina ilikuwa inaongoza kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili Saudi Arabia walicheza mchezo wa kushambulia kwa kushtukiza pamoja na kucheza mtindo wa kutegea kuotea (Offside Trick) na kufanikiwa kupata mabao mawili yaliyofungwa na Al-Shehir katika dakika ya 49 pamoja na AlDawsari katika dakika ya 53.

Katika mchezo huo jumla ya wachezaji sita (6) wa Saudi Arabia walipewa kadi za njano huku Argentina ikiwa haijapewa kadi hata moja.

Kwa matokeo hayo Saudi Arabia inaongoza kundi ikiwa na jumla ya alama 3 huku Argentina ikiburuza mkia kwa kuwa na point 0 ikiwa imebakiwa na michezo miwili.

SOMA NA HII  GAMONDI:- TUTACHEZA PIRA 'VANILA' KWENYE MECHI ZA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA...